WANAFUNZI 2,679 WAPATA MIKOPO ELIMU YA JUU KUPITIA RUFAA
HomeJamii

WANAFUNZI 2,679 WAPATA MIKOPO ELIMU YA JUU KUPITIA RUFAA

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TAARIFA KWA UMMA WANAFUNZI 2,679 WAPATA MIKOPO YA TZS 9.6 BILIONI KUPITIA RUFAA Jumann...

RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KENYATTA WA KENYA, JIJINI KAMPALA UGANDA.
PROFESA JOHN SHAO AZUNGUMZIA UZOEFU WAKE KATIKA MASUALA YA TIBA: NI KWENYE SEMINA YA WCF KWA MADAKTARI
RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO MAALUM WAKUU WA NCHI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) UNAOFANYIKA KAMPALA NCHINI UGANDA

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAARIFA KWA UMMA
WANAFUNZI 2,679 WAPATA MIKOPO YA TZS 9.6 BILIONI KUPITIA RUFAA
Jumanne, Disemba 5, 2017
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Disemba 5, 2017) imetangaza orodha yenye wanafunzi 2,679 ambao wamepata mikopo ya elimu ya juu yenye thamani ya TZS 9.6 bilioni kufuatia kukamilika kwa uchambuzi wa rufaa zilizowasilishwa na wanafunzi hao.
Kati ya wanafunzi hao, 1,847 ni wa mwaka wa kwanza ambao mikopo yao ina thamani ya TZS 6.84 bilioni na wengine 832 ni wale wanaoendelea na masomo lakini hawakuwa na mikopo katika miaka iliyopita. Wanafunzi hao wanaoendelea na masomo wamepata mikopo yenye thamani ya TZS 2.76 bilioni.


Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru

Orodha kamili ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kupitia dirisha la rufaa inapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz) na fedha za wanafunzi hao zimetumwa katika vyuo walipo wanafunzi hao hivi sasa.
Hatua hii inafanya jumla ya wanafunzi 33,200 wa mwaka wa kwanza kuwa wamepangiwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya TZS 108 bilioni kwa mwaka wa masomo 2017/2018 hadi sasa. Bajeti ya jumla kwa wanafunzi wote kwa mwaka 2017/2018 ni TZS 427.54 bilioni.
Dirisha la rufaa lilifunguliwa kwa siku saba kuanzia tarehe 13 Novemba, 2017 hadi tarehe 19 Novemba, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawakuwa wameridhika na upangaji wa mikopo na kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili.
Wanafunzi waliohamishiwa mikopo yao
Wakati huohuo, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imeanza kuhamisha mikopo iliyokuwa imeelekezwa katika vyuo tofauti na waliko kwa sasa. Mikopo ya wanafunzi 590 wa mwaka wa kwanza yenye thamani ya TZS 1.78 bilioni ambayo awali ilikuwa imepelekwa katika vyuo tofauti na walipo wanafunzi imehamishwa.
Wanafunzi hao waliohamishiwa mikopo yao ni wale ambao walipangiwa mikopo na kupelekewa fedha zao katika vyuo ambavyo walipata udahili awali, ila baadaye wakaamua kujiunga na vyuo vingine ambavyo nako walipata udahili.
Orodha kamili ya wanafunzi hao pamoja na fedha za wanafunzi hao zimetumwa katika vyuo walipo hivi sasa.
Bodi ya Mikopo inaendelea kupokea orodha za wanafunzi waliosajiliwa katika vyuo mbalimbali na wale wenye mikopo, fedha zao zitahamishiwa katika vyuo walipo katika awamu zijazo.
Mikopo kwa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu
Aidha, jumla ya wanafunzi 45 wa shahada za uzamili na uzamivu ambao ni wanataaluma na waajiriwa wa vyuo mbalimbali nchini wamepata mikopo yenye thamani ya TZS 441.4 milioni katika mwaka wa masomo 2017/2018.
Mikopo hii hutolewa na Bodi ya Mikopo kwa wanataaluma hao ili kuvijengea vyuo uwezo wa kitaaluma chini ya makubaliano kati ya Bodi ya Mikopo na vyuo hivyo.
Imetolewa na:

Abdul-Razaq Badru
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Jumanne, Disemba 5, 2017

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANAFUNZI 2,679 WAPATA MIKOPO ELIMU YA JUU KUPITIA RUFAA
WANAFUNZI 2,679 WAPATA MIKOPO ELIMU YA JUU KUPITIA RUFAA
https://lh5.googleusercontent.com/AUL8W58vNnpm6HbtVntqwe0qaf6TjHYrgoe4E_TqrraIoSU2TuUWD3-Nb4N1iW3Dr-w5k5OyBcIqHGSsr28ct5nonqsVU7BiKACMEAw6eES0qQdCYTK5fNB3VsbiAnupyXpRdjyVo0dPM-ZLxw
https://lh5.googleusercontent.com/AUL8W58vNnpm6HbtVntqwe0qaf6TjHYrgoe4E_TqrraIoSU2TuUWD3-Nb4N1iW3Dr-w5k5OyBcIqHGSsr28ct5nonqsVU7BiKACMEAw6eES0qQdCYTK5fNB3VsbiAnupyXpRdjyVo0dPM-ZLxw=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/wanafunzi-2679-wapata-mikopo-elimu-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/wanafunzi-2679-wapata-mikopo-elimu-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy