WAFUGAJI BUKOMBE MKOANI GEITA WAWALALAMIKIA ASKARI WANYAMA PORI LA AKIBA KIGOSI

Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wamewalalamikia askari wa pori la Akiba la Kigosi Myobosi kwa madai ya ku...


Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, wamewalalamikia askari wa pori la Akiba la Kigosi Myobosi kwa madai ya kuwanyanyasa pindi wanapokamata ng'ombe zao katika pori hilo. 

Wakiongea mwishon mwa wiki ,mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Hamisi Ulega,wafugaji hao wamesema kuwa Mifugo yao inauzwa bila kufuata utaratibu pindi inapokamatwa kwenye pori hilo na matokeo yake wafugaji wanabaki Maskini. 

"Magufuli anafanya kazi nzuri sana na hatuamini kabisa kuwa hapendi Mifugo,lakini kuna baadhi ya watendaji wake sio waadilifu kabisa, askari wa pori la akiba Kigosi Myobosi wakikamata ng'ombe hawatupi fursa ya kulipa faini, badala yake wanataifisha Mifugo yetu na kuipiga mnada bila kufuata utaratibu wa serikali uliowekwa na sisi tunabaki Maskini"alisema mfugaji mmoja. 

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Mkoa wa Geita Bw. Hamisi Mashaka Biteko ameiomba serikali kutafuta masoko ya uhakika ya mifugo Ili wafugaji wewe na uhakika wa soko la Mifugo yao. 

"Tunaomba serikali ijenge viwanda vya kutosha vya kuchakata nyama Ili wafugaji wenye Mifugo mingi waweze kuuza Mifugo yao,inayobaki wafuge kwa tija" 

Kwa Upande wake naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla Ulega amesema kuwa Sheria ya Maliasili na utalii inaruhusu kupigwa mnada Mifugo yote inayoingia kwenye mapori ya akiba. lakini wamepeleka mswada Bungeni ili kuzipitia upya sheria hizo .

"Katika Bunge la mwezi wa pili 2018,sheria hizo zitapitiwa upya,nawaombeni sana ikifika wakati huo mjipange vizuri nanyi mtoe maoni yenu" 

Awali katibu tawala wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Bw.Paul Cheyo, akitoa taarifa fupi ya Wilaya hiyo alimwambia Mhe.Ulega kuwa wao wametekeleza zoezi la kitaifa la upigaji chapa mifugo kwa Asilimia 73. 

"Halmashauri inaendelea na zoezi la upigaji chapa mifugo.Wilaya yetu ina jumla ya ng'ombe 130,750, hadi sasa ng'ombe waliopigwa chapa ni 95,743 sawa na asilimia 73".alisema Cheyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kupokea taarifa fupi ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla Ulega akizungumza na viongozi mbalimbali na wafungaji Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
.Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Mkoa wa Geita Bw.Hamisi Mashaka Biteko (kushoto)akizungumza katika mkutano huu.
Mmoja wa wa wafungaji wa akitoa kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdalla Ulega, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.

Sehemu ya viongonzi mbalimbali na wafungaji waliofika katika mkutano huo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAFUGAJI BUKOMBE MKOANI GEITA WAWALALAMIKIA ASKARI WANYAMA PORI LA AKIBA KIGOSI
WAFUGAJI BUKOMBE MKOANI GEITA WAWALALAMIKIA ASKARI WANYAMA PORI LA AKIBA KIGOSI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgT8jWay6U5u7AXb6c3f7p5Qx8-kcmTIUprrIhD_IFQ0WvhNIX2_Q4bY7bsVg1QRbQu2LZGvg14ob99wZXOpUHx379H4nsSgtpVETZjHAneih0AvFZjXVLHZtLDDU5ZGF0it1wb4NVphPL9/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgT8jWay6U5u7AXb6c3f7p5Qx8-kcmTIUprrIhD_IFQ0WvhNIX2_Q4bY7bsVg1QRbQu2LZGvg14ob99wZXOpUHx379H4nsSgtpVETZjHAneih0AvFZjXVLHZtLDDU5ZGF0it1wb4NVphPL9/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/wafugaji-bukombe-mkoani-geita.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/wafugaji-bukombe-mkoani-geita.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy