Kaimu Mganga Mkuu wa serikali Dk. Mohamed Mohamed akifungua mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala leo jiji...
|
Kaimu Mganga Mkuu wa serikali Dk. Mohamed Mohamed
akifungua mkutano wa Baraza la wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam waliokutana kujadili mafanikio, changamoto na mipango mbalimbali waliyonayo katika utoaji wa hudumabora za afya kwa wananchi.
|
|
Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Tiba za Asili na Tiba Mbadala wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Paulo Mohammed akitoa ufafanuzi wa hali halisi ya Tiba za Asili na Tiba mbadala nchini Tanzania na mpango wa serikali wa kuendelea kuthamini huduma inayotolewa na wataalam hao.
|
|
Baadhi ya wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala waliohudhuria mkutano wa Baraza la Wataalam wa tiba hiyo wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo.
|
|
Mratibu wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala kutoka Shirika la
Afya Duniani (WHO) Rose Shija akisoma salam za mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania Dk. Rufaro Chatora ambaye amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kutatua changamoto zinazowakabili wataalam wa Tiba za Asili na Tiba mbadala.
|
|
Mtafiti mwandamizi mkuu wa Idara ya Utafiti wa Tiba Asili kutoka Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu Hamis Masanja Malebo akitoa mada kuhusu historia ya Tiba za Asili na uhusiano uliopo katika matumizi ya mimea ya asili kati ya tiba za asili na tiba mbadala na tiba za kisasa katika utengenezaji wa dawa. (Picha na Aron Msigwa - MAELEZO)
|
COMMENTS