RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA DODOMA
HomeJamii

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA DODOMA

Usiku wa Kitendawili kufufua upya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dr John Pombe Magufuli an...

UJUMBE WA RAIS MSTAAFU MZEE BENJAMINI WILLIAM MKAPA KWA VYOMBO VYA HABARI
CCM ZANZIBAR YAWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO
RAIS MAGUFULI AMUANDALIA DHIFA YA KITAIFA MHENI WAKE, RAIS JACOB ZUMA WA AFRIKA KUSINI

Usiku wa Kitendawili kufufua upya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dr John Pombe Magufuli anataraji kuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ utakaofanyika Ijumaa hii Disemba 8 2017 kupitia ‘Usiku Wa Kitendawili’ mjini Dodoma.

Akizungumza na Waandishi wa habari Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ndio wataouratibu usiku huo wa Kitendawili kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Sanaa utamaduni na Michezo.

Usiku wa Kitendawili ulianzishwa baada ya msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kuachia wimbo ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo.

Akiongea na wadau wa sanaa katika Maandalizi ya Kampeni hiyo ya Kitaifa itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, Mrisho Mpoto amesema kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza ndani ya Taifa letu.

Alisema mambo ambayo yatayozingatiwa katika kampeni hiyo ni pamoja na kudhubiti na hatimaye kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma, kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka ufisadi, ubadhilifu wa mali za Umma pamoja kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.

“Usiku wa Kitendawili utatumika kama jukwaa la kuwaleta pamoja watanzania pamoja na viongozi wao ili kukumbushana kuhusu wajibu na kujadili mustakabali wa Taifa. Kutakuwa na vivutio mbalimbali pamoja na wimbo maalumu kutoka kwa wasanii maalumu Mwaka Huu,” alisema Mpoto.

Aliongeza,”Tumekuja kuunadi Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ kwasababu tunaamini Uzalendo na Utaifa lazima uwepo ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kuunga mkono juhudi za Raisi Dkt. John Pombe Magufuli za kujenga Taifa lenye Uzalendo, Utu, Weledi na Uadilifu uliotukuka. Mimi ni mzalendo ndio maana hata kwenye hizi harakati nipo toka nimetoa wimbo wangu wa kwanza, ukiangalia nyimbo zangu zote ni za kuonganisha jamiii 120 za watanzani,”

“Naamini kwenye kufanya kazi ambayo itawafanya watanzania pamoja na kizazi kijacho kitambue kuna watu ambao walifanya kazi kubwa kwenye hili taifa, kuacha alama ambazo haziwezi kufutika katika maisha ya historia ya nchi hii, kwa sababu hivi vyote ambavyo vinaenda kufanywa ni kufufua upya na kuiweka pamoja mitazamo ya watanzania ili kujenga Taifa la Wazalendo na Wachapakazi kuiga nyayo zilizoachwa na hayati Baba wa Taifa,” alifafanua zaidi.

Mpoto amesema lengo kuu la maadhimisho hayo kuambatana na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa kuanzia mwaka 2018 ni kutumia jukwaa hilo kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kujenga na kuendeleza Utaifa.

Alisema baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo wiki hii huko Dodoma, itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni chini ya Uwenyekiti wa Mkuu wa Mkoa na Wilaya.



--
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA DODOMA
RAIS MAGUFULI MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiijdu926Ot1t60NGJ4s4fGJhrH3YH_OseWX9RxoyfuU2Mna6IKvW6Ds9-hJcO83KKPeyotoWJp7huKP5FI6R1_WiPce2Hkq1jA8yg2sYD5sxTW_VIaPjv1UcTmAGc6PI179kcCqrfvLd8/s640/d92cfc12-39d4-4a2c-a4af-17cbaefe8201.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiijdu926Ot1t60NGJ4s4fGJhrH3YH_OseWX9RxoyfuU2Mna6IKvW6Ds9-hJcO83KKPeyotoWJp7huKP5FI6R1_WiPce2Hkq1jA8yg2sYD5sxTW_VIaPjv1UcTmAGc6PI179kcCqrfvLd8/s72-c/d92cfc12-39d4-4a2c-a4af-17cbaefe8201.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/rais-magufuli-mgeni-rasmi-uzinduzi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/rais-magufuli-mgeni-rasmi-uzinduzi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy