Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge ali...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Disemba, 2017 amewasili Mkoani Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru zitakazofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi tarehe 09 Desemba, 2017.
Katika Ikulu ya Chamwino, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Satano Mahenge.
Akiwa Mkoani Dodoma Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) atafungua vikao vya Jumuiya za CCM na pia atakuwa mgeni rasmi katika shughuli mbalimbali za kiserikali.
Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
07 Disemba, 2017
COMMENTS