POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora WP Nina Dachi wa kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi)
HomeJamii

POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU.

Na Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi nchini limewaonya badhi ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na...

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI
BENKI YA CRDB NA JESHI LA MAGEREZA KUEDELEA KUBORESHA UHUSIANO WA KIBIASHARA
AIRTEL NA VETA WASHIRKIANA KUANDAA KONGAMANO LA ELIMU KUPITIA MTANDAO



Na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limewaonya badhi ya watumishi wasio waaminifu wanaofanya kazi katika Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)  ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta na miundombinu mbalimbali ya shirika hilo kuacha mara moja.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi Mwandamizi PATRICK BYATAO wakati wa hafla fupi ya kuwatunukia zawadi baadhi ya Askari waliofanya vizuri katika kuhakikisha usalama wa miundombinu ya shirika hilo ambapo baadhi yao walifanikiwa kuwakamata watumishi wa shirika hilo wakiiba mafuta.
Amesema katika siku za karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watumishi wa shirika hilo wasio waaminifu ambapo wamekuwa wakilitia hasara shirika hilo jambo ambalo amesema wanaendelea kuimarisha usalama ili kuhakikisha kuwa wanawadhibiti.
BYATAO amesema Kikosi hicho kitaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha wanakomesha tabia hiyo ambayo imekuwa ikidhoofisha utendaji wa TAZARA pamoja na kuitia hasara Serikali.
Akizungumzia utoaji wa Zawadi hizo BYATAO amesema askari hao kumi wamefanya vizuri kwa kujituma katika kipindi cha mwaka 2017 hivyo kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi ni vyema kuwazawadia ili kuongeza morali yao ya kazi na kuwafanya wengine kuendelea kujituma zaidi.
Kwa upande wake mmoja wa Askari waliopata zawadi baada ya kufanya vizuri WP NINA DACHI amewaasa askari wenzanke kuendelea kufanya kazi kwa umakini ili kuhakikisha kuwa miundominu ya shirika hilo inakuwa salama wakati wote.


Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi cheti cha utendaji bora mmoja wa askari wa  kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akimkabidhi zawadi ya jiko la gesi mmoja wa askari wa  kikosi hicho baada ya kufanya vizuri katika kazi zake ambapo alifanikisha kuzuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha TAZARA Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi Patrick Byatao akikagua gwaride wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku askari waliofanya vizuri kwa mwaka 2017 katika kikosi hicho ambapo kwa kiasi kikubwa wamezuia wizi wa mafuta katika reli ya TAZARA. (Picha na Jeshi la Polisi)


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU.
POLISI TAZARA WATOA ONYO KWA WAHALIFU.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBY_lTWEXUl4H2DLH1uX2MiUoMtMVsoastLlCKnnKdHMC0ZGJzVuvVdcpU94mW-MQYHJL67-rHx092shyphenhyphenjRGl_vhCdGHpkR0mvnbdO4QOuaz_l8c498fdbzjh1rAzb3kOnKezPzymlXIQ/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBY_lTWEXUl4H2DLH1uX2MiUoMtMVsoastLlCKnnKdHMC0ZGJzVuvVdcpU94mW-MQYHJL67-rHx092shyphenhyphenjRGl_vhCdGHpkR0mvnbdO4QOuaz_l8c498fdbzjh1rAzb3kOnKezPzymlXIQ/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/polisi-tazara-watoa-onyo-kwa-wahalifu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/polisi-tazara-watoa-onyo-kwa-wahalifu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy