NAIBU WAZIRI MADINI ATEMBELEA MACHIMBO YA JASI MKOANI SINGIDA

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akishuhudia upakiaji wa Madini ya Jasi katika kijiji cha Kihanju, Itigi yanayosafirishwa kuelekea kwenye Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement ikiwa ni moja ya malighafi ya kutengenezea Saruji.


HomeJamii

NAIBU WAZIRI MADINI ATEMBELEA MACHIMBO YA JASI MKOANI SINGIDA

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo hapo jana alifanya ziara kwenye machimbo ya Jasi (Gypsum) ya Mkoani Singida na kuzungumza na Waf...

RC MAKONDA AWATAKA WAKUU WA WILAYA WOTE KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KISHERIA
TANZIA:TANGAZO LA KIFO CHA MZEE XAVERY MIZENGO PINDA
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS FIDEL CASTRO WA CUBA

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo hapo jana alifanya ziara kwenye machimbo ya Jasi (Gypsum) ya Mkoani Singida na kuzungumza na Wafanyabiashara na Wachimbaji wa Madini hayo ambapo aliwahakikishia ushirikiano wa dhati wa kufikia malengo waliyojiwekea.
Alitembelea maeneo ya machimbo ya Madini ya Jasi na Viwanda vidogo vya uongezaji thamani ya madini hayo ikiwemo viwanda vya kusaga madini ya Jasi ambayo unga wake unasafirishwa nje ya Mkoa huo, viwanda vya kutengeneza chaki vilivyopo Itigi na kiwanda cha utengenezaji wa mapambo ya majumbani kilichopo Singida Mjini.
Naibu Waziri Nyongo yupo Mkoani Singida kwenye ziara ya siku Tatu ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uchimbaji wa madini Mkoani humo ili kujionea shughuli zinazofanywa kwenye maeneo hayo na kuzungumza na wachimbaji wa madini ili kubaini changamoto zinazowakabili kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wake.
Kwa mujibu wa wachimbaji wa madini hayo, Madini ya Jasi hutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kutengenezea chaki, hospitalini kwa watu waliovunjika na kutengeneza viungo bandia, kutumika kutengenezea saruji, urembo majumbani, hutumika kama insulation kwenye majengo makubwa kwa kuwa Jasi huzuia moto, kutengenezea midoli na masanamu, kutengeneza meno bandia na pia hutumika kama mbolea


Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akiwasikiliza wachimbaji na wafanyakazi wa machimbo ya Jasi, yaliyopo katika Kijiji cha Kihanju, Itigi, Mkoani Singida alipofanya ziara kwenye machimbo hayo.




Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akitazama hatua ya uchomaji wa Madini ya Jasi kwenye kiwanda cha kampuni ya mzawa cha RSR kilichopo katika Kijiji cha Sanjaranda, Itigi kabla ya kusagwa kuwa unga na baadaye kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzwa na mwingine kutumika katika Kiwanda cha kutengenezea mapambo ya Majumbani, katika kiwanda kilichopo Singida mjini.




Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akikagua mitambo ya kusagia mawe ya Madini ya Jasi kwenye Kiwanda cha kutengeneza Chaki cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha Majengo, Itigi.




Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akitazama Chaki zinazozalishwa na Kiwanda cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha Majengo, Itigi ambazo huuzwa ndani na nje ya Mkoa huo huku lengo likiwa ni kuuza nje ya Tanzania.




Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha kutengeneza Chaki cha Furaha, kilichopo katika Kata ya Tambukareli, Itigi, Peter Nolasco (kulia) akielezea namna Madini ya Jasi yanavyosagwa na kuwa unga (Gypsum powder) kwa ajili ya kutengenezea Chaki. 


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAIBU WAZIRI MADINI ATEMBELEA MACHIMBO YA JASI MKOANI SINGIDA
NAIBU WAZIRI MADINI ATEMBELEA MACHIMBO YA JASI MKOANI SINGIDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfCH08vxVdqiDK5-hrvfyb3oZwS_ImmuDZcmnhW5LvwXJKZpT5FwiVYOF9_120egFcWpFIlaIxKe_Ku78gQfcirkDXTVWiqEC-aGCYoquS40enzVCF2mKA1d0jSxrzZIeNr6fCbHWpoCY/s640/MBILI+.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfCH08vxVdqiDK5-hrvfyb3oZwS_ImmuDZcmnhW5LvwXJKZpT5FwiVYOF9_120egFcWpFIlaIxKe_Ku78gQfcirkDXTVWiqEC-aGCYoquS40enzVCF2mKA1d0jSxrzZIeNr6fCbHWpoCY/s72-c/MBILI+.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-madini-atembelea-machimbo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/naibu-waziri-madini-atembelea-machimbo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy