RAIS MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS FIDEL CASTRO WA  CUBA
HomeJamii

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS FIDEL CASTRO WA CUBA

 Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro enzi za uhai wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe...

BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
JARIDA LA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU - MEI, 2017.
NGUVU KAZI YA TAIFA INATEKETEA KWA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA- RC DODOMA






 Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro enzi za uhai wake




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016.
Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema;

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia, Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu.

Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika.
Naungana nawe na wananchi wa Cuba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, na pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe, familia na wananchi wote wa Cuba muwe na nguvu, subira na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu."

Pia Rais Magufuli amemuombea marehemu Fidel Castro apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Novemba, 2016
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS FIDEL CASTRO WA CUBA
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS FIDEL CASTRO WA CUBA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgJkD6Zb6kEpleCIfxJ1nrx0TBQSw0adwT6LNw3Ch1caZrCz0affT_u7MhweKFnhtwNWc9eknOSimzUBUIESRCTOEWBFleJTbw0YMS74aqJxihZ5oRd9ZRo10moodx9ciUq6CgC3GifF9kS/s640/048A5A5A0000044D-0-image-a-4_1431291777643.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgJkD6Zb6kEpleCIfxJ1nrx0TBQSw0adwT6LNw3Ch1caZrCz0affT_u7MhweKFnhtwNWc9eknOSimzUBUIESRCTOEWBFleJTbw0YMS74aqJxihZ5oRd9ZRo10moodx9ciUq6CgC3GifF9kS/s72-c/048A5A5A0000044D-0-image-a-4_1431291777643.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/rais-magufuli-atuma-salam-za-rambirambi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/rais-magufuli-atuma-salam-za-rambirambi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy