Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku ya jana ilikuwa ni zamu ya wilaya ya Kinondoni. ...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku ya jana ilikuwa ni zamu ya wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza
na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni RC Makonda ametoa agizo kwa Wakuu
wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga
marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wamekuwa
wanaitumia kinyume na utaratibu kwa kudhulumu haki za wanyonge ikiwemo
kuuza viwanja kinyume na utaratibu, huku akisisitiza kuwa watendaji wa
mtaa ndiyo inabidi wakae na mihuri hiyo.
Pia RC
Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha
kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na
kuwashauri wananchi kabla ya kuipeleka mahakamani na kuwaweka wazi kama
kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.
Katika
hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard
Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa
wakati ili kuharakisha maendeleo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia
watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea
maendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) akizungumza na
watumishi wa Manispaa ya Kinondoni ambapo ametoa agizo kwa Wakuu wote
wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga
marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wanaitumia
kinyume na utaratibu, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na Kamanda wa Polisi wa Kanda
Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza machache na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipokea ripoti ya Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwasili kwenye ukumbi wa Police
Officer’s Mess akiambatana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jijini Dar es Salaam.
COMMENTS