Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kisare Makori akihutubia washiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Siku 16 za kupin...
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kisare Makori akihutubia washiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoandaliwa na TGNP Mtandao.
MKUU wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kisare Makori leo amezinduwa kampeni ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoandaliwa na TGNP Mtandao, zikiwa na ujumbe wa kutambua mchango wa klabu za jinsia katika harakati za kupinga ukatili wa jinsia.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Makori alisema kiwango cha ukatili wa kijinsia nchini na duniani bado ni kikubwa, kwani taarifa ya afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria Tanzania ya mwaka 2015/16 inaonesha kuwa wanawake wanne kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.
Alisema takwimu hizo zinaonesha kuwa asilimia 42 waliowahi kuolewa wamekumbana na ukatili wa wenza wao ama wa kimwili au ukatili unaohusiana na kingono. "Hivyo basi nawaomba Watanzania wenzangu katika maeneo yenu pazeni sauti na kufanya kwa vitendo kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia unaowakumba sana wanawake na watoto," alisisitiza Mkuu wa Wilaya, Bw. Makori.
Awali akizungumza kabla ya hotuba ya mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Grace Kisetu alisema lengo kuu la kampeni za mwaka huu kwao ni kushirikisha mawazo na uzoefu wa shule katika harakati za kumlinda mtoto wa kike ndani na nje ya shule dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Alisema mengine ni pamoja na kutambua mchango wa klabu za jinsia katika harakati za kupinga ukatili wa kijinsia, kutumia michezo au sanaa katika kuwezesha kampeni za kupambana na ukatili wa kijinsia, elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.
[caption id="attachment_83196" align="aligncenter" width="500"]
COMMENTS