MAPENDEKEZO YA MUSWAADA WA KUTOA TAARIFA YAFIKA PAZURI

MAPENDEKEZO YA MUSWAADA WA KUTOA TAARIFA YAFIKA PAZURI Imeelezwa kuwa kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi kutapunguza uhalif...



MAPENDEKEZO YA MUSWAADA WA KUTOA TAARIFA YAFIKA PAZURI
Imeelezwa kuwa kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi kutapunguza uhalifu unaohatarisha amani na kuongeza usalama wa mtu, jamii, nchi na dunia kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, amesema hayo katika kikao cha wadau cha kupitia mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi na kusisitiza umuhimu wa kujielimisha kabla ya kusambaza taarifa.
“Ni muhimu kwa jamii kuelewa haki ya faragha ya mtumiaji wa mawasiliano na namna ya kushughulikia taarifa katika ukusanyaji, usambazaji, uchakataji na uhifadhi ili kuepuka kutenda uhalifu” amesema Dkt. Sasabo.
Dkt. Sasabo amezungumzia umuhimu wa jamii kuzingatia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na sheria ya miamala ya kielektroniki ya mwaka 2015 ili kuepuka makosa yasiyo yalazima na kuepuka usambazaji wa taarifa binafsi za watumiaji wa mawasiliano usiouwiana na maadili na wenye nia ovu.
“Ni vema jamii ikajua mitandao haina mipaka, hivyo ni muhimu kuwa na muongozo utakaosimamia haki za watumiaji na kulinda taarifa binafsi”, amesisitiza Dkt. Sasabo.
Naye, Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Bi. Eunice Masigati, amesema mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamechangia ongezeko kubwa la makosa katika mawasiliano ya simu na intaneti hivyo uwepo wa sheria inayosimamia taarifa binafsi utapunguza changamoto za kimtandao na kuongeza haki ya faragha.
Dkt. Sasabo, alikuwa katika kikao kazi cha wadau kukusanya maoni ya mapendekezo ya kutungwa sheria ya kulinda taarifa za watumiaji ili kupunguza uhalifu na kuhakikisha usalama wa taarifa binafsi.
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)


Wadau wa Sekta mbalimbali, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (hayupo pichani), wakati wa mkutano wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi,Mkoani Dodoma, leo.



Afisa Sheria wa Sekta ya Mawasiliano, Eunice Masigati, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Usalama Mtandao, Eng. Stephen Wangwe.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma, leo.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wadau walioshiriki katika mkutano wa siku moja wa maoni kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi, Mkoani Dodoma.





COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAPENDEKEZO YA MUSWAADA WA KUTOA TAARIFA YAFIKA PAZURI
MAPENDEKEZO YA MUSWAADA WA KUTOA TAARIFA YAFIKA PAZURI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7c-fPznGOSNkupYcSJsKsKDPXqqNkvwfLyT7s397priQJhGyiWi99nwi4qypD4iV0uI77VSHegi_KRrcaYgUkvl83fr91AODfjX20Jb5QTLevk44p2T46Vhyphenhyphen825NS1PwadYgv4R8wMt8/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7c-fPznGOSNkupYcSJsKsKDPXqqNkvwfLyT7s397priQJhGyiWi99nwi4qypD4iV0uI77VSHegi_KRrcaYgUkvl83fr91AODfjX20Jb5QTLevk44p2T46Vhyphenhyphen825NS1PwadYgv4R8wMt8/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/mapendekezo-ya-muswaada-wa-kutoa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/mapendekezo-ya-muswaada-wa-kutoa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy