NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari MWANASOKA nyota wa zamani wa AC Milan, George Opong Weah, ametangazwa mshindi wa kiti cha Rais wa Liber...
NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
MWANASOKA nyota wa zamani wa AC Milan, George Opong Weah, ametangazwa mshindi wa kiti cha Rais wa Liberia, kwenye uchaguzi wa marudio uliomalizika hivi karibuni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Liberia, imesema leo Desemba 29, 2017 kuwa Weah ameshinda kwa asilimia 61.5 ikiwa ni jumla ya asilimia 98.1 ya kura zilizopigwa na kuhesabiwa na kumuacha mpinzani wake, Makamu wa Rais, Joseph Boakai akiambulia asilimia 38.5 ya kura.
Kwa matokeo hayo, George Weah anachukua mikoba ya Rais aliyemaliza muda wake, Bi. E;len Johnson Sirleaf na anatarajiwa kuapishwa mwezi ujao.
Weah mwenye umri wa miaka 51 amekulia katika familia masikini nchinin Liberia, na alilelewa na mama yake mkubwa katika eneo wanakoishi masikini kwenye mji mkuu Monroavia.
Hata hivyo Weah alionekana kuwa ni kipaji cha hali ya juu cha kusakata soka katika miaka ya 90.
Alicheza soka kwenye timu kadhaa za Afrika kabla ya kuelekea barani Ulaya na kuchezea timu ya Monaco ya nchini Ufaransa, iliyokuwa chini ya kocha wa sasa wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger.
Wea alikuwa mwanasoka wa kwanza na pekee hadi sasa kutoka Afrika, aliyefanikiwa kushinda Mwanasoka bora wa Dunia wa FIFA na tuzo ya Ballon d’Or.






COMMENTS