UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO KUPITIA MSHIPA WA DAMU WA MKONO (CATHETERIZATION) WAFANYIKA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA MARA YA KWANZA

Na Mwandishi wetu,   16/11/2017 Jumla ya wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji wa  kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa ...



Na Mwandishi wetu,

 16/11/2017 Jumla ya wagonjwa 20 wamefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa upasuaji wa aina hiyo kufanyika hapa nchini.



Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge alisema upasuaji huo unafanyika  katika kambi ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na madakatari kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya  Misaada (IIRO) ya nchini Saudi  Arabia.
Dkt. Kisenge alisema kuwa kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu na kubadilishana ujuzi wa kazi  kati ya wafanyakazi wa Taasisi hizo mbili ikiwemo aina mpya ya upasuaji wanaoufanya kitu ambacho kinawajengea uwezo zaidi. ”
“Faida ya upasuaji huu ni kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa anatembea na baada ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri anaweza kuruhusiwa.
 “Tofauti na upasuaji wa kutumia mshipa wa paja ambao tulikuwa tunaufanya, baada ya upasuaji mgonjwa ni lazima akae Hospitali kwa zaidi ya masaa 24 ili kuangalia maendeleo ya afya yake”, alisema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake  Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya IIRO Ali Al Masoud   alisema kambi hiyo inaendelea vizuri kwani kwa siku wanatibu wagonjwa 10 na baada ya matibabu afya zao zinaimarika tofauti na ilivyokuwa  kabla ya matibabu.
Dkt. Masoud aliongeza kuwa  wamekuja na utaalam mpya wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono ambapo kabla ya hapo matibabu yaliyokuwa yanafanyika ni ya kutumia mshipa wa damu wa kwenye paja.
Alifafanua, “Hivi sasa tunafanya upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua  kitu ambacho wenzetu hawa walikuwa wanakifanya. Sisi tumewaongeza utaalam mpya wa kutumia mshipa ya mkononi badala ya mshipa wa  paja.
Naye Bader Alanezi ambaye ni Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu kutoka IIRO alimalizia kwa kusema kuwa  wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na kupata uzoefu mpya  wa baadhi ya magonjwa na mambo ya kiteknolojia ambayo katika nchi yao hakuna.

Jumla ya wagonjwa  40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano ambayo imeanza tarehe 14 hadi tarehe 18 mwezi huu.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO KUPITIA MSHIPA WA DAMU WA MKONO (CATHETERIZATION) WAFANYIKA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA MARA YA KWANZA
UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO KUPITIA MSHIPA WA DAMU WA MKONO (CATHETERIZATION) WAFANYIKA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA MARA YA KWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4vqM7RchK3wIA3o3v5OClNuxSTioYzIIy-J8BMrVncr_dlXVMEbzOzLN3gXSLPEFDb3BhuHeH_PhL9RH5kNokdPA65gPsP8xLC2Ja3_HOzzShq6gdPPH72gxsP6smd6_Ji2v980dYDHNo/s400/_DSC0566.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4vqM7RchK3wIA3o3v5OClNuxSTioYzIIy-J8BMrVncr_dlXVMEbzOzLN3gXSLPEFDb3BhuHeH_PhL9RH5kNokdPA65gPsP8xLC2Ja3_HOzzShq6gdPPH72gxsP6smd6_Ji2v980dYDHNo/s72-c/_DSC0566.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/upasuaji-wa-kuzibua-mishipa-ya-moyo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/upasuaji-wa-kuzibua-mishipa-ya-moyo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy