TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU SIFA NA TAKWIMU ZA UTOAJI MIKOPO KWA 2017-2018
HomeJamii

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU SIFA NA TAKWIMU ZA UTOAJI MIKOPO KWA 2017-2018

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TAARIFA KWA UMMA UFAFANUZI KUHUSU UPANGAJI MIKOPO KWA 2017/2018 Novemba 6, 2017 Bod...

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA TRIONI MOJA KUTOKA GLOBAL FUND KUSAIDIA TB,UKIMWI NA MALARIA
WAZIRI MBARAWA AUFUNGUA MKUTANO WA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) JIJINI DAR ES SALAAM
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA DKT. WILBROAD SLAA IKULU DAR ES SALAAM


BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU UPANGAJI MIKOPO KWA 2017/2018
Novemba 6, 2017
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu sifa na taratibu za utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018. Taarifa hii inalenga kutoa ufafanuzi kufuatia maoni ya baadhi ya wadau kuwa baadhi ya waombaji mikopo wenye sifa wanakosa mikopo ya elimu ya juu.
  1. Uyatima: Waombaji ambao wamefiwa na wazazi na hivyo kushindwa kumudu gharama za elimu ya juu. Kwa mwaka huu, waombaji yatima wanapaswa kuthibitisha uyatima wao kwa kuwasilisha vyeti vya vifo vya wazazi wao vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA);


  1. Wenye ulemavu: Waombaji wa mikopo wenye ulemavu wanapaswa kuambatisha barua kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa inayothibitisha ulemavu huo;


  1. Uduni wa kipato: Waombaji ambao wanatoka kwenye familia zenye vipato duni, miongoni mwao wakiwamo wale wenye barua za uthibitisho kuwa waliosomeshwa kwenye masomo yao kabla ya kujiunga na elimu ya juu;


Pamoja na sifa/vigezo hivi, kila mwombaji ni lazima awe amepata udahili au kuthibitisha udahili katika taasisi moja ya elimu ya juu ambayo atajiunga kwa ajili ya masomo na asiwe na umri wa zaidi ya miaka 30.


Aidha, tunapenda kufafanua kuhusu takwimu za utoaji mikopo kwa mwaka 2017/2018 kama ifuatavyo:
  1. Bajeti ya jumla ya mikopo kwa mwaka 2017/2018 ni TZS 427.54 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 122,623. Fedha hizi zinajumuisha malipo ya ada za wanafunzi wenye mikopo pamoja na fedha za chakula na malazi, vitabu n.k;
  2. Fedha zinazohitajika kwa malipo kwa ajili ya Robo ya Kwanza ya mwaka 2017/2018 ni TZS 147.06 bilioni ambazo tayari Bodi imeshapokea kutoka Serikalini;
  3. Hadi leo, Novemba 6, 2017, jumla ya wanafunzi 29,578 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 96.5 bilioni na fedha zao tayari zimeshatumwa vyuoni ili kuwawezesha kuanza masomo;
  4. Aidha, fedha za mikopo ya wanafunzi wote wanaoendelea na masomo zimetumwa vyuoni ili kuwawezesha kuendelea na masomo.
Kufunguliwa kwa dirisha la rufaa
Tunapenda pia kuwajulisha waombaji wa mikopo wote kuwa dirisha la rufaa litafunguliwa Jumatatu, Novemba 13, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili. Maelezo ya kina yatatolewa kupitia tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).


Tunatoa wito kwa uongozi wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafuzi na kuwasilisha kwa Bodi ya Mikopo. Lengo ni kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa rufaa zao ifikapo Novemba 30, 2017.


Imetolewa na:


(Signed)


Abdul-Razaq Badru
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Novemba 6, 2017

HESLB EXECUTIVE DIRECTOR - ABDUL BADRU

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU SIFA NA TAKWIMU ZA UTOAJI MIKOPO KWA 2017-2018
TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU SIFA NA TAKWIMU ZA UTOAJI MIKOPO KWA 2017-2018
https://lh5.googleusercontent.com/24QzbRozI9S4fKRJKSBJnAq1nIzrTc6BQdS2WL7B1EzP17YA_644yhz-v4V4xXe9mB9u1e-mcfuAVaR5KJm-cC1XIs_njFwa1ilZ7bA6kPopKfHHrE7rknMtxcJpVh8m4yg11m77dTyigQZVCQ
https://lh5.googleusercontent.com/24QzbRozI9S4fKRJKSBJnAq1nIzrTc6BQdS2WL7B1EzP17YA_644yhz-v4V4xXe9mB9u1e-mcfuAVaR5KJm-cC1XIs_njFwa1ilZ7bA6kPopKfHHrE7rknMtxcJpVh8m4yg11m77dTyigQZVCQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/taarifa-ya-ufafanuzi-kuhusu-sifa-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/taarifa-ya-ufafanuzi-kuhusu-sifa-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy