KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO
HomeJamii

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO

Dar es Salaam, Novemba 15.2017 Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam inatarajia kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi w...

MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA VALERIE NDENEINGO AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA RADIO NA TELEVISION ZA MTANDAONI ( ONLINE RADIO NA TELEVISION) DAR
THE GUARDIAN LIMITED NAYO YAJISALI MAELEZO; DKT. ABAS AWASIHI WENGINE WASISUBIRI MUDA WA KUFANYA HIVYO KUISHA
UDHIBITI WA UBORA WA MAZAO SULUHISHO LA USALAMA WA CHAKULA


Dar es Salaam, Novemba 15.2017

Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam inatarajia kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo mkoani Pwani siku ya jumapili ya tarehe 19.2017.Kambi hiyo ya siku moja itatoa vipimo vya afya, ushauri, matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili, minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi na kwa mara ya kwanza itaendesha vipimo vya kansa ya shingo ya uzazi

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa kambi ya matibabu Bwana Frédéric Morel amesema amefurahishwa na maandalizi ya mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita.
“Tumefurahishwa na ushirikiano tunaopata kutoka kwa makampuni na watu binafsi katika kuhakikisha kambi hii inafanyika kwa mara nyingine tena.pili, tunatarajia idadi ya watu kuwa mara mbili kulinganisha na mwaka uliopita”.Alisema, Morel.
mbali na kambi ya Kerege, klabu yetu pia mwaka huu imetoa huduma ya matibabu ya bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msasani A. Hivyo tunaomba wakazi wa Kerege na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.” Frédéric Morel.

Kwa upande wake Rais wa klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam, Anne Saels,
amesema kuwa kuwa kambi hii ni mfano wa huduma Za Rotary kwa jamii.

“kutoa huduma za afya kwa watu takribani 2000 hufanywa pindi watu wanaojitolea kukutana pamoja na kushirikiana kufanya kazi ili kubadilisha maisha ya wengine kuwa bora. Mwisho, uhalali wetu kama Rotary hupimwa kwa na huduma tunayotoa na tunajivunia kuwa na uwezo wa kuandaa Matibabu ya Matibabu mwaka baada ya mwaka”.Alisema, Anne Saels.

Mbali na hilo, Mwakilishi kutoka benki ya Diamond Trust, Bwana Sylvester Bahati amesema ushirikiano na klub ya Rotary ya Oyster Bay katika miaka mitano iliyopita umekuwa ni ushrikiano mzuri wenye kubadili maisha ya watu.

“Mpaka sasa zaidi ya watu 1000 wamepatiwa huduma bora za kiafya katika kambi hii na kuhimiza watu kujitolewa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika jamii zao.Jeshi la wafanyakazi wa matibabu litakalo kusanyika siku ya tarehe 19.11.2017 haliwezi kupatikana popote kama kikundi wakati wowote ule, hii inafanya kambi ya matibabu ya Kerege kuwa ya kipekee na takribani watu 25 kutoka benki ya DTB hujitolea kila mwaka katika kambi.”Alisema ,Bwana Sylvester Bahati.

Kambi hii ya matibabu itafanyika kwa udhamini wa benki ya Diamond Trust, Whitedent, kampuni ya vinywaji ya Peps, Securex , ICAP kutoka chuo cha Colombia, pamoja na madakatri na wanafunzi kutoka Chuo cha kumbukumbu cha Herbert Kairuki, chuo kishirikishi cha afya cha MUHAS, na makundi mbalimbali kutoka asasi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali.

Klabu ya Rotary ya Oysterbay imeanzishwa mwaka 2009 na kwasasa ina wanachama 62. Ni klabu kubwa kati ya klabu 7 za rotary zinazopatikana Dar es Salaam. Klabu ya Rotary imekuwa ikiisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali baadhi yake kati ya hiyo miradi ni pamoja na Kambi ya matibabu kwa shule ya Msasani , Mradi wa vijana Poa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rotary Dar Marathon, “Rotary Mission Green” mradi wa kupanda miti, na kwasasa Rotary inajiandaa kuja na mkakati mpya utakaofanya kazi ya kuiisaidia jamii moja kwa katika maeneo mbalimbali tofauti na huduma za afya.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO
KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY DAR KUTOA MATIBABU YA BURE KWA WAKAZI WA KEREGE BAGAMOYO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8y5lu9_QLLC2CX1I2z6Z7ZJ1arL7cjV1iwE0zCcdn2Ih5I1iyEGpFwTft_mqJSRWua8oQVMZ_nlqjhWQ6mT9DoAkC3sEmCT1xYa-QUXYchRM11natKq09RtqNu7t0uBzjKv-aY9VtMAgo/s640/pic.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8y5lu9_QLLC2CX1I2z6Z7ZJ1arL7cjV1iwE0zCcdn2Ih5I1iyEGpFwTft_mqJSRWua8oQVMZ_nlqjhWQ6mT9DoAkC3sEmCT1xYa-QUXYchRM11natKq09RtqNu7t0uBzjKv-aY9VtMAgo/s72-c/pic.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/klabu-ya-rotary-ya-oyster-bay-dar-kutoa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/klabu-ya-rotary-ya-oyster-bay-dar-kutoa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy