Shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani WoteSawa lenye makazi yake Jijini Mwanza, leo limezindua mradi wa kuwajengea uwez...
Shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani WoteSawa lenye makazi yake Jijini Mwanza, leo limezindua mradi wa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa nyumbani katika Manispaa ya Ilemela ili kutetea haki na maslahi yao.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo uitwao “Paza Sauti ya Mfanyakazi wa Nyumbani”, Mkurugenzi wa shirika hilo Angel Benedicto amesema mradi huo pia utawasaidia wafanyakazi wa nyumbani kufichua changamoto zinazowakabiri.
Mkurugenzi wa WoteSawa, Angel Benedicto akizungumza kwenye uzinduzi na utambulisho wa mradi huo uliofanyika Monarch Hotel Mwanza.












COMMENTS