MULTICHOICE YAJA NA OFA KABAMBE YA FUNGA MWAKA NA DSTV

Dar es Salaam Jumatano November 15, 2017;  Kama ilivyo ada, katika msimu huu wa sikukuu, Multichoice tanzania imetangaza neema kwa watanzan...


Dar es Salaam Jumatano November 15, 2017; Kama ilivyo ada, katika msimu huu wa sikukuu, Multichoice tanzania imetangaza neema kwa watanzania kwa kutoa ofa kabambe kwa wateja wake ambapo kuanzia leo mteja mpya wa DStv ataweza kuunganisha kwa shilingi 79,000 tu hii kikiwa ni vifaa vyote pamoja na kifurushi cha DStv Bomba cha mwezi mzima.




Balozi maalum  wa DStv, Nancy Sumari akizungumza wakati wa hafla maalum ya kutangazwa kwa  punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei zitakazoanza kutumika rasmi Septemba mosi 2017.

Akizungumzia ofa hiyo, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo, amesema kuwa Multichoice imekuwa na utamaduni wa miaka nenda rudi wa kuwapa zawadi wateja na watanzania kwa ujumla na kwamba kila ufikapo msimu kama huu DStv huwatunuku wateja wake ili kuwawezesha kufurahia zaidi msimu huu wa sikukuu.
Tunafahamu kuwa msimu huu wa sikukuu familia nyingi zinaungana katika kusherehekea, hivyo DStv imeamua kuwaongezea burudani kwa kutoa ofa hii kabambe. Amesema badala ya mteja mpya kulipa shilingi 98,000 kwa ajili ya kuunganishwa pamoja na kifurushi cha mwezi, sasa watalipa shilingi 79,000 tu na kuunganishwa na DStv pamoja na kifurushi cha Bomba cha mwezi mzima.
“Tunapokuwa nyumbani na familia zetu, watoto wanataka waangalie katuni, sisi kinamama tunapenda kuangalia vipindi kama vile vya mapishi, urembo, na tamthilia, kinababa nao hupenda sana kutazama michezo mbalimbali kama kandanda na kadhalika. Ni kwa msingi huu tumeamua kuwarahisishia burunani hii inayopatikana kutoka DStv” alisema Hilda na kuongeza kuwa wataendelea kutoa ofa kwa wateja wao kila inapihitajika.
Ofa hii ni kwa nchi nzima na itaendelea kwa miezi miwili hadi Januari 15, 2018
Ofa hii kwa wateja wapya inakuja siku chache tu baada ya DStv kuanza kutoa zawadi kwa wateja wake kwa kuwaongezea chaneli za SuperSport kwenye vifurushi vyao punde walipiapo akaunti zao kabla hazijakatika.
Katika ofa hii ya kuongezewa chanel, wateja wa kifurushi cha Compact na Compact Plus watapata chaneli zote za SuperSport zinazopatikana katika kifurushi cha DStv Premium kwa kipindi cha siku saba (7) mfululizo bureeee!
Hali kadhalika, watumiaji wa  kifurushi DStv Bomba  na DStv Family  nao watapata chanel zote za Supersport zinazopatikana kwenye Kifurushi DStv Compact na hivyo kuweza kushuhudia mechi zote za Ligi ya Uingereza (PL) na mashindano mengine makubwa kwa siku saba (7) mfululizo bureee!
Multichoice Tanzania imekuwa ikitoa huduma za DStv hapa nchini kwa Zaidi ya miaka 20 sasa na imeendelea kuwa kinara katika kuwapatia watanzania habari, elimu na Zaidi ya yote burudani kabambe.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MULTICHOICE YAJA NA OFA KABAMBE YA FUNGA MWAKA NA DSTV
MULTICHOICE YAJA NA OFA KABAMBE YA FUNGA MWAKA NA DSTV
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOOPUp9jSs3bDUgBs3QX769qGcaJ1VrGiv-VlMi1Xz49gZ55PxVuDADK4sLyUiTC7iqXNA-fk-SxVwogUBPQnVfLRBmxTXJ0pM1d4zF3bG29CGrpE135MlIAEoGvq1WAHZSA903FOL1ls/s640/Nancy+Sumari.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOOPUp9jSs3bDUgBs3QX769qGcaJ1VrGiv-VlMi1Xz49gZ55PxVuDADK4sLyUiTC7iqXNA-fk-SxVwogUBPQnVfLRBmxTXJ0pM1d4zF3bG29CGrpE135MlIAEoGvq1WAHZSA903FOL1ls/s72-c/Nancy+Sumari.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/multichoice-yaja-na-ofa-kabambe-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/multichoice-yaja-na-ofa-kabambe-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy