MTANDAO WA UTEPE MWEUPE (WHITE RIBBON) WAZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MAORE JUUU YA VIFO VTOKANAVYO NA UZAZI KWA KINAMAMA NA WATOTO WACHANGA.

Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa  (The White Ribbon Alliance ) Rose Mlay akizungumza na wananchi katika kijiji cha Maore wil...


Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa  (The White Ribbon Alliance ) Rose Mlay akizungumza na wananchi katika kijiji cha Maore wilayani Same wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Taasisi ya Utepe mweupe (White Ribbon)  kujadili vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Mganga Mkuu wa wilaya ya Same,Dkt Godfrey Andrew akizungumza wakati wa mkutano na wananchi ulioandaliwa na Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon) kujadili  vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Mkutano ukiendelea katika jengo la Mahakama lililopo katika kijiji cha Maore wilayani Same.
Baadhi ya kina mama wakiwa na watoto wao katika mktano huo.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Maore wilayani Same wakichangia wakati wa mkutano uliondaliwa na Mtandao wa White Ribbon kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

WANANCHI katika kijiji cha Maore wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro,wamesema tatizo la vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga vinachangiwa na upungufu wa watumishi katika zahanati ya kijiji pamoja na ufinyu wa wodi ya wazazi iliyopo.

Wakitoa maoni yao katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Taasisi ya Utepe mweupe (White Ribbon)  kujadili vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga katika kijiji cha Maore wilayani Same wananchi hao wameiomba serikali kuangalia namna ya kutatua changamoto hizo.

Mbali na changamoto hizo wakazi wa Maore wameeleza pia changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wa kike kupata ujauzito pindi wawapo shuleni kuna changiwa na wazazi kushindwa kuwaeleza ukweli  watoto wao kuhusu kuanza mahusiano wawapo shuleni .

Mganga Mkuu wa wilaya ya Same ,Dkt Godfrey  Andrew amesema vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga vimepungua wilayani Same hadi kufikia 15 mwaka huu ukilinganisha na vifo 60 vilivyotokea katika miaka miwili iliyopita ya 2015 na 2016 huku akibainisha mikakati iliyopo ya kupambana na changamoto za upungufu wa watumishi.

Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa  (The White Ribbon Alliance ) Rose Mlay amesema  kuwekeza kwa mama mjauzito kunachangia kuzaliwa kwa kijana mwenye afya njema atakayechangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kulea maendeleo.

Same ni mojawapo ya wilaya saba zilizoko katika mkoa wa Kilimanjaro zinazokabiliwa na changamoto ya vifo vya akina mama wajawazito vitokanavyo na uzazi huku sababu ya vifo hivyo kwa kina mama ikielezwa kuwa ni Kifafa cha Mimba,kupasuka kwa mji wa mimba na kutokwa na damu nyingi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MTANDAO WA UTEPE MWEUPE (WHITE RIBBON) WAZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MAORE JUUU YA VIFO VTOKANAVYO NA UZAZI KWA KINAMAMA NA WATOTO WACHANGA.
MTANDAO WA UTEPE MWEUPE (WHITE RIBBON) WAZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MAORE JUUU YA VIFO VTOKANAVYO NA UZAZI KWA KINAMAMA NA WATOTO WACHANGA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisG7YE2dafLR9OvuxfbZqBZ55t0GtRPpwbG5s3nroIh-rKBgybw7hBd2Hbj9oWHLOsYa77JrK3MZvCxAMhkDrRje1q2lBDo5yHY4EXUXx9VCVIFoCf1YyqSOtZsY9IW-fQSSH0avLx6um7/s640/E86A3510.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisG7YE2dafLR9OvuxfbZqBZ55t0GtRPpwbG5s3nroIh-rKBgybw7hBd2Hbj9oWHLOsYa77JrK3MZvCxAMhkDrRje1q2lBDo5yHY4EXUXx9VCVIFoCf1YyqSOtZsY9IW-fQSSH0avLx6um7/s72-c/E86A3510.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/mtandao-wa-utepe-mweupe-white-ribbon.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/mtandao-wa-utepe-mweupe-white-ribbon.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy