MATUKIO MBALIMBALI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI - MNAZI MMOJA DSM

NA WAMJW-DA ES SALAAM. WATANZANIA waaswa kujihusisha na tabia ya kupenda kufanya mazoezi ili kuepuka ugonjwa wa kisukari na viashir...



NA WAMJW-DA ES SALAAM.

WATANZANIA waaswa kujihusisha na tabia ya kupenda kufanya mazoezi ili kuepuka ugonjwa wa kisukari na viashiria vyake  katika jamii yetu inayotuzunguka.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya afya Dkt. Neema Rusibamayila alipomwakilsha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa  kuadhimisha siku ya Kisukari duniani leo jijini Dar es salaam.

“Watanzania tunatakiwa kupenda kujijengea tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweza kuepuka magonjwa yasioambukiza ikiwemo Kisukari na viashiria vyake kwa ujumla” alisema Dkt. Rusibamayila.

Aidha Dkt. Rusibamayila amesema kuwa  watanzania wengi hawana  budi kujikinga na ugonjwa huo kwani asilimia 60 wanafariki kwa ugonjwa huo duniani kila mwaka.

Kwa mujibu Wa Dkt. Rusibamayila amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake nchini wana uzito mkubwa,mafuta mengi na hawajihusishi na mazoezi hivyo hupelekea kupata hathari za ugonjwa wa kisukari.

Mbali na hayo Dkt. Rusibamayila  amesema kuwa licha tu ya kufanya mazoezi lakini pia wanatakiwa kuepuka matumizi ya vileo kama vile uvutaji tumbaku,unywaji pombe na uvutaji wa shisha ili kuepuka magonjwa yasioambukiza kwani yamekuwa hatari kwa watanzania.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Vicent Assey amesema kuwa sambamba na kufanya mazoezi watanzania wanatakiwa kuzingatia mlo ulio bora ili kuepuka ugonjwa wa kisukari.

Aidha Dkt Assey amesisitiza  walimu , wazazi na watoa huduma ngazi ya jamaii wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha watoto na jamii nzima kwa ujumla juu ya lishe bora ambayo huleta kinga zidi ya kisukari.

Siku ya kisukari Duniani huadhimshwa Novemba 14 kila mwaka na mwaka huu imeadhimishwa sambamba na matembezi ya hiari na mazoezi ya pamoja kutoka viwanja vya muhimbili mpka Mnazi mmoja na kubeba Kauli mbiu isemayo “MWANAMKE NA KISUKARI “ ikimaanisha wanawake wawe mstari wa mbele katika kupambana na ugonjwa huo.

Watumishi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya  Dkt. Vicent Assey (aliyevaa tisheti ya bluu) mapema leo katika matembezi ya Siku ya Kisukari Duniani yaliyoanza chuo cha Muhimbili mpaka Viwanja vya Mnazi mmoja. (Imeandaliwa na Robert Okanda)

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa Umma (HEU) Said Makora (kushoto) akimsikiliza  Mkurugenzi msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi wakati wa maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.


Watumishi  na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya wakinyoosha viungo baada ya matembezi yaliyo anzia Chuo cha Muhimbili na kukomea viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam katika maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani huku kauli mbiu ikiwa  ni Wanawake na Kisukari.


Mkurugenzi wa kituo cha Lishe na Chakula Wizara ya Afya  Dkt. Vicent Assey akitoa neno mbele ya wadau wa Afya na Ugonjwa wa Kisukari (Hawapo kwenye picha) wakati wa maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Kinga  Dkt. Neema Rusibamayira ambae alimwakilisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu akisoma taarifa mbele ya wadau wa Afya na Kisukari nchini (hawapo kwenye picha) katika maazimisho ya Siku ya Kisukari Duniani ambayo kikomo chake ni Novemba 14. Wakwanza  kushoto ni Dkt Waane na wa mwisho ni Mkurugenzi msaidizi wa NCD Wizara ya Afya Dkt. Sara Maongezi.


Picha ya pamoja ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kinga  Dkt. Neema Rusibamayira katika  maazimisho ya Siku ya Kisukari Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.



Watumishi  na Wadau mbali mbali wa masuala ya Afya wakishiriki matembezi yaliyo anzia Chuo cha Muhimbili na kukomea viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam katika maazimisho ya siku ya Kisukari Duniani huku kauli mbiu ikiwa  ni Wanawake na Kisukari.




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MATUKIO MBALIMBALI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI - MNAZI MMOJA DSM
MATUKIO MBALIMBALI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI - MNAZI MMOJA DSM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4pUq-h23ofDamFUrHk8Y8fOz8ZiroNWT6CcBLANvpoDm64Q4rGZD1wHDkGzq-AroXGRHoZcBdMXawrY3v_Y-af2aYpsxLq4iBZ2bHGsgbqY8inPoyz3ilS4kSLylm9EImtlRXfGJXCWE/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4pUq-h23ofDamFUrHk8Y8fOz8ZiroNWT6CcBLANvpoDm64Q4rGZD1wHDkGzq-AroXGRHoZcBdMXawrY3v_Y-af2aYpsxLq4iBZ2bHGsgbqY8inPoyz3ilS4kSLylm9EImtlRXfGJXCWE/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/matukio-mbalimbali-ya-maadhimisho-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/matukio-mbalimbali-ya-maadhimisho-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy