MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA
HomeJamii

MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS Nchini akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Magerez...

TCAA KUBORESHA MIUNDOMBINU UONGOZAJI NDEGE
JARIDA LA NCHI YETU MWEZI SEPTEMBA
KATIBU MKUU MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO BIBI SIHABA NKINGA AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA KWA MAAFISA USTAWI WA JAMII NCHINI MJINI DODOMA.



Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS Nchini akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) alipowasili kwenye katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo 30 Novemba, 2017 hapa mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia Ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma..

Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha.

Mjumbe wa Mkutano huo ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremiah Nkondo akichangia mada katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara .

Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiteta jambo na Mgeni rasmi Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde kama inavyoonekana katika picha.

Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(waliosimama). Walioketi(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos anayemaliza muda wake, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili toka kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano unaofanyika kwa siku moja Mkoani Dodoma(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).




Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS) kimefanya Mkutano wake Mkuu wa Tano wa Mwaka 2017 kwa ufanisi Mkoani Dodoma.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Miyuji Dodoma leo Novemba 30, 2017.


Akiongea katika Mkutano huo Kaimu Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde kwa niaba ya Naibu Mrajisi ametoa angalizo kwa Vyama vya ushirika nchini kutokufanya biashara za Kibenki nje ya lengo la kuanzishwa kwa SACCOS.


Amesema kuwa katika vyama vingi vya ushirika uzoefu umeonesha kuwa wakishakuwa na mtaji mkubwa huwa na wazo la kuanzisha Benki, ametoa angalizo kuwa masharti ya uendeshaji wa Benki ni tofauti kabisa na masharti ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hivyo ameziasa Saccos zote nchini kutafakari vyema kabla ya kubadili vyama hivyo na kuwa Benki.
“ Ukianzisha Benki huduma za Saccos zitafifia, kumbukeni wateja wa Saccos ni pamoja na wale wa hali ya chini kabisa ikiwa benki hawa huenda mkawaacha” alisisitiza Kaimu Mrajis Malunde.


Aidha, amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria lakini pia kuheshimu na kusikiliza sana wenye mali ambao ni wanachama wa vyama hivyo vya ushirika.


Aliongeza kuwa kwakuwa Mkutano huu utahusisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi Bw. Charles Malunde pia amewaasa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua watu wenye weledi na wenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili waweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.


Pia amewataka wagombea wote wanaowania nafasi mbalimbali za chama hicho kujiuliza mambo manne kama ifuatavyo;- Je, watumishi wa Jeshi la Magereza wote ni wanachama? na mnaweka Mkakati gani?, Je wanachama wanaweka akiba za kila mwezi?, Mnajiendesha kisayansi? Mtu akitaka mkopo anapata baada ya muda gani? na swali la mwisho uhusiano na vyama vingine vya ushiriki, SCULT, nje ya nchi ukoje?.


Awali akitoa taarifa ya Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS), Mwenyeki wa Bodi ya Magereza Saccos, DCP. Gideon Nkana amesema kuwa Idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 18.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA
MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRDis7XkXRX0ZKz9Kx-XoWWMzFK5v_ruGr0vpR1rMzJ1gAqrEN70_5QtX5ar5rcfI479lN2Ro46EVsk3osMwCvYfbPvWAy9SP477ovzPgeE9hZHuJmZ3ZvMk9wHmR3V-QGJv0H0XcBPrLG/s640/PIX+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRDis7XkXRX0ZKz9Kx-XoWWMzFK5v_ruGr0vpR1rMzJ1gAqrEN70_5QtX5ar5rcfI479lN2Ro46EVsk3osMwCvYfbPvWAy9SP477ovzPgeE9hZHuJmZ3ZvMk9wHmR3V-QGJv0H0XcBPrLG/s72-c/PIX+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/magereza-saccos-yafanya-mkutano-mkuu-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/magereza-saccos-yafanya-mkutano-mkuu-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy