DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017
HomeJamii

DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe, (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensh...

NAIBU WAZIRI MHE .JULIANA SHONZA AKARIBISHWA OFISINI MAKAO MAKUU, DODOMA
DKT TIZEBA AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI





Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe,
(kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
wakiwaonyesha waandishi wa habari, tuzo ambayo PSPF ilinyakua katika mashindano
ya kimataifa wakati wa mkutano wa taasisi ya hifadhi ya jamii Duniani, International social security association,
taasisi tanzu ya ILO, tuzo ya ISSA GOOD
PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017
mjini Adis Ababa Ethiopia mwezi
uliopita. Tukio hili limefanyika pembezoni mwa mkutano wa kampeni ya uzalendo
na utaifa iliyoongozwa na waziri Mwakyembe kwenye ukumbi wa mikutano wa PSPF
jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2017.


NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said




MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umenyakua tuzo ya kimataifa ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS
AFRICA COMPETITION 2017, baada ya kuwa Mfuko unaotoa huduma bora kupitia
ubunifu wa mafao ya muda mfupi, yaani service
quality in short-term products.


Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kuonyesha tuzo hiyo iliyokwenda sambamba na kampeni ya
uzalendo na utaifa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu alisema, Mfuko huo
unajivunia kwa kuwa Mfuko wa kwanza miongoni mwa Mifuko mitano ya Hifadhi ya
Jamii nchini, kuanzisha bidhaa na huduma za muda mfupi ambazo zimekuwa kivutio
kikubwa kwa wanachama na hivyo kuvutia mifuko mingine ambayo kwa sasa nayo
imeanza kutoa huduma hizo.


“Mwaka
huu katika mkutano wake wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani yaani
International Social Security Association, taasisi tanzu ya Shirika la Kazi
Duniani,(ILO) imeipatia PSPF tuzo baada ya kuwa Mfuko bora barani Afrika katika utoaji huduma bora kupitia ubunifu wa Mafao ya
muda mfupi yaani service quality kwenye short-term products.” Alifafanua Bw.
Mayingu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison
Mwakyembe aliipongeza PSPF kwa kujinyakulia tuzo hiyo na kuliletea taifa
heshima kubwa kimataifa.
“Kupambanishwa
katika bara la Afrika na kushinda vigezo kadhaa ndipo unaambiwa bwana wewe
unapata hii tuzo na tuzo hii imetolewa na taasisi yenye ushirikiano wa karibu
sana na ILO hongereni sana.” Alipongeza Dkt. Mwakyembe.
Alisema
ushirikiano wa karibu miongoni mwa wafanyakazi wa PSPF ndio umepelekea
mafanikio hayo.
“Niwapongeze
viongozi wote wa PSPF, Wafanyakazi wote wa PSPF, kwa kazi nzuri mnayoifanya
mpaka mnatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa.” Alisema.
Aidha
kabla ya tukio hilo, Waziri aliwahamasisha watanzania kujenga moyo wa uzalendo
na kujivunia utaifa wao kwani mambo hayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa.
“Sisi
tuliokuwepo kabla ya uhuru, niwaombe sana, tuwasaidie vijana wetu wa sasa
kutambua tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi, kwa kujenga uzalendo wa
kuipenda nchi yetu kama ambavyo ilikuwa hapo awali.” Alisema.


Kampeni
hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muunganmo wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao mjini Dodoma, na Waziri
aliwahamasisha wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia fedha ili kufanikisha
swala hilo muhimu kwa taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyemba, akizungumza kuhusu umuhimu wa jamii kiujenga uzalendo wa taifa lao la Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Leah Kilimbi, akizungumzia maudhui ya hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. ASdam Mayingu, akizunhgumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakayti wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw.Sami Khalfan, wakifuatilia hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Nelly Msuya akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa vipindi wa Azam TV, Bw. Charles Hillary, (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Bw. Mayingu akizungumza huku akipongezwa kwa makofi na waziri Mwakyembe na Bi.Joyce Fisso, Katibu Mtendaji bodi ya Filamu Tanzania.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bi. Grace Michael Kisinga.




Baadhi ya wageni waalikwa
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fisso, akizungumza.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017
DKT. MWAKYEMBE AIPONGEZA PSPF KWA KUTWAA TUZO YA KIMATAIFA YA ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017
https://i.ytimg.com/vi/DzYXy_WVl9s/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/DzYXy_WVl9s/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/dkt-mwakyembe-aipongeza-pspf-kwa-kutwaa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/dkt-mwakyembe-aipongeza-pspf-kwa-kutwaa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy