Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Waajiri wote nchini yakiwemo makampuni ya Madini wametakiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya ...
Na Daudi
Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Waajiri wote
nchini yakiwemo makampuni ya Madini wametakiwa kutekeleza matakwa ya Sheria ya
kazi kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi.
Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera Bunge Ajira Kazi na watu wenye Ulemavu
Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini
Dodoma.
“Makampuni
haya yana wajibu mkubwa wa kulinda haki za wafanyakazi,kupunguza migogoro isiyo
ya lazima sehemu za kazi na kuongeza tija na uzalishaji mahala pa
kazi.”Aliongeza Mhe.Mavunde.
Aidha amesema
Ofisi yake imeendelea kutekeleza majukumu yake ya usimamizi wa Sheria kwa
kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa waajiri wanazingatia
matakwa ya Sheria,elimu ya Sheria za kazi inatolewa kwa waajiri,wafanyakazi na
vyama vyao ili kuongeza uelewa wao katika kutekeleza Sheria.
Kuhusu ukaguzi
wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini amesema Serikali iliunda kikosi ambacho
kilishirikisha Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, NSSF, SSRA,OSHA ,Mamlaka ya
Mapato Tanzania na Wakala wa Ukaguzi wa Madini.
Amesema kikosi
kazi hiki kilipewa jukumu la kufanya ukaguzi wa kina kwenye migodi iliyopo
kanda ya ziwa na kaskazini kwa lengo la kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa
Sheria za kazi,afya na usalama mahali pa kazi,masuala ya hifadhi ya jamii,fedha
na kodi.
Pamoja na hayo
amesema kuwa Serikali inatambua umhimu wa uwekezaji katika kukuza fursa za
ajira kwa watanzania na kuchangia kukua uchumi kwa ujumla.
“Serikali
itaendelea kusimamia sheria za kazi ili kuhakikisha kuwa waajiri wote nchini
wanatimiza wajibu wao na wawekezaji wamepata nafasi ya kuwekeza na kuchangia
kukua kwa uchumi wa nchi yetu kwa kufuata sheria zilizoko nchini”Alisisitiza
Mhe. Mavunde.
COMMENTS