Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akiwasili ...
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akiwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kalemie, Kongo kwa ajili ya kushiriki mkutano wa
kubadilishana data na uzoefu kuhusu mafuta katika Tanganyika
uliofanyika hivi karibuni nchini Kongo. Nchi nyingine zilizoshiriki ni
pamoja na Burundi, Kongo na Zambia. Wengine kutoka kushoto ni Gavana wa Jimbo la Tanganyika
– Kongo, Richard Ngoy Kitangala, Waziri wa Migodi na Madini Nchini
Zambia, Chris Yaluma na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia
ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) na Gavana wa Jimbo la Tanganyika
– Kongo, Richard Ngoy Kitangala (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa
yanatolewa na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo,
Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa (hayupo pichani) katika mkutano huo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Sheria, Wizara ya Nishati na Madini, Anna Ngowi (kushoto)
pamoja na wataalam wengine kutoka Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akiweka mchanga kwenye jiwe
la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi
katika mji wa Kalemie. Kulia kwake ni Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya
Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka kushoto, mbele) pamoja
na viongozi wengine wakishikana mikono kama ishara ya umoja mara baada
ya kuzindua ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi katika mji wa Kalemie hivi karibuni .
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa tatu kushoto mbele) na
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime
Ngoi-Mukena Lusa ( wa sita kulia mbele) wakiwa katika picha ya
pamoja na watendaji wengine mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi katika mji wa Kalemie hivi karibuni.
Mtaalam
kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Athur
Lyatuu (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wajumbe wa mkutano
huo.
Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa katika mkutano huo.
COMMENTS