Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef, Peter Zizhou (kulia) akielezea teknolojia ya zamani ya uchenjuaji wa dhahabu kwa Waziri...
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef, Peter Zizhou (kulia) akielezea teknolojia ya zamani ya uchenjuaji wa dhahabu kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) mara alipofanya ziara kwenye mgodi huo uliopo mkoani Geita kwa ajili ya kujionea maendeleo ya shughuli zake tarehe 27 Oktoba, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Na Greyson Mwase, Geita
Oktoba 27, 2017
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amesema
Serikali inatarajia kuwasilisha majina ya wananchi 1062 waliofanyiwa tathmini katika eneo la Kiseme wilayani Geita
ili kulipwa fidia kwa ajili ya kupisha
shughuli za uchimbaji madini za Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef katika Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kufanyiwa uhakiki na kubaini uhalali
wa umiliki wake kabla ya kuanza kwa taratibu za malipo.
Waziri Kairuki aliyeambatana na Naibu Waziri
wa Madini, Stanslaus Nyongo ameyasema hayo mapema leo katika Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef uliopo
wilayani Geita mkoani Geita mara baada
ya kuhitimisha ziara yake ya siku moja katika mgodi huo ili kujionea
maendeleo ya mgodi huo na kutatua
changamoto zake.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara zake pamoja
na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus
Nyongo katika migodi ya serikali, binafsi na wachimbaji wadogo katika mikoa
ya Kagera na Geita ili kufahamu kwa
undani mafanikio na namna ya kutatua
changamoto zilizopo katika sekta ya
madini.
Alisema kuwa, kabla ya kuanza kwa ulipaji wa
fidia, ni lazima Wizara ya Madini ihakikishe majina ya wanaodai fidia
yanafikishwa katika Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki na wataalam wa
wizara hiyo ili kuepuka udanganyifu
kwenye umiliki wa ardhi.
Aliendelea kusema kuwa katika sekta ya madini
kumekuwepo na migogoro mingi hususan katika
madai ya fidia kutokana na wamiliki wengi wasiokuwa halali kujitokeza na kudai fidia
hali inayochangia wawekezaji
kushindwa kulipa kutokana na gharama kuwa kubwa.
Katika hatua nyingine, Kairuki alitaka
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lenye umiliki wa asilimia 45 katika
mgodi huo kwa niaba ya Serikali kuhakikisha linafanya tathmini ya
vifaa vyote vinavyotumika katika uchimbaji na uchenjuaji madini pamoja na
mikataba kati yake na mbia wake ambaye
ni kampuni ya Tanzam 2000 mwenye asilimia 55.
“Mkumbuke kuwa mmepewa dhamana na Serikali ya kusimamia mgodi huu, hivyo ni jukumu
lenu kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa yanaangaliwa huku mkifanya kazi kwa
ubunifu wa hali ya juu ili uchimbaji
ulete tija,” alisema Kairuki.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza katika kikao na uongozi na wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Busolwa Mining Limited, alisema
kuwa Serikali ipo tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo ili uzalishaji wao ulete manufaa kwenye uchumi wa nchi.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano
imejipanga katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wa madini hususan wazawa
wanafanya shughuli zao katika mazingira
rafiki na kupata faida kubwa na kutoka kwenye lindi la umaskini
Alisisitiza wachimbaji wa madini kufuata
kanuni na sheria katika shughuli zao na kuongeza kuwa Serikali kupitia Wizara
ya Madini itaendelea kutoa elimu kuhusu kanuni na sheria za madini.
WANAODAI FIDIA MGODI WA BUCKREEF KUHAKIKIWA
Advertisement

MAIN QUOTE
x cbfgmfg hghg
- Steve Jobs
WEEK TRENDING
Loading...
YEAR POPULAR
HUYU NDIYE MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KULIKO WOTE DUNIANI MWANAMA Mikel Ruffinelli mkazi wa Los Angeles, Marekani, amedhihirisha k...
Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha Meja Jenerali Paul Mssao akitoa taarifa ya maofisa wapya kwa Amiri ...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza...
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kufunga mafunzo ya ...
Msomaji wa Quran tukufu katika mashindano ya kitaifa, Abdallah Abdulkadri akisoma wakati wa fainali zake mashindano Dar es Sal...
COMMENTS