Na Genofeva Matemu –WHUSM Oktoba 23/2017 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amevitaka vyombo ...
Na Genofeva
Matemu –WHUSM
Oktoba 23/2017
Naibu Waziri
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amevitaka
vyombo vya habari vya serikali kufuata maadali na miiko ya uandishi wa habari kwa
kuzingatia weledi ili umma eweze kupata habari zilizokidhi vigezo vya uandishi
wa habari.
Rai hiyo
ameitoa jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Kampuni ya Magazeti
ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na kuzungumza
na watendaji wa taasisi hizo.
“Vyombo vya
habari vya serikali viwe mfano bora kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa
watanzania wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kwani vyombo hivi ni moja kati
ya mhimili mkubwa wa nchi na kama vitatumika vibaya madhara yake ni makubwa
sana” amesema Mhe. Shonza
Aidha Mhe.
Shonza amesema kuwa Serikali inathamini na kutambua mchango unaotolewa na
vyombo vya habari vikiwemo vyombo vya serikali TBC katika kufikisha taarifa za
ukweli na uhakika katika jamii.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba amemhakikishia
Mhe. Shonza kuwa TBC itaendelea kuzingatia weledi na maadili katika kuhabarisha
umma huku ikiendelea kubuni vipindi mbalimbali vitakavovutia jamii kuangalia
televisheni hiyo.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa TSN
imeendelea kuhakikisha kuwa taifa linahabarishwa kwa hakika kwa kutumia nyenzo
mbalimbali na uzoefu tangu ilipoanzishwa miaka 88 iliyopita hivyo kuchangia katika
maendeleo ya nchi yetu
“kwa sasa TSN
ni zaidi ya magazeti, imejikita zaidi kuwa kampuni inayotoa huduma za habari
kwa kutumia nyenzo mbalimbali za kiteknolojia ili kuweza kuendana na kasi ya
maendeleo ya sayansi na taknolojia” amesema Dkt. Yonazi.
 |
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya
Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati)
alipofanya ziara katika Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim Yonazi
|
 |
Mkurugenzi Mtendaji TSN Dkt. Jim
Yonazi akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza katika Kampuni hiyo jana Jijini
Dar es Salaam
|
 |
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na
Menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara katika
Kampuni hiyo jana Jijini Dar es Salaam
|
 |
Mhariri wa gazeti la Daily News Bw.
Leonard Mwakalebela (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) namna habari
zinavopitiwa na kupangwa katika gazeti hilo alipofanya ziara katika kampuni ya
TSN jana Jijini Dar es Salaam
|
 |
Meneja wa uchapishaji wa magazeti ya
Serikali Bw. Boniface Mwajombe (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) mpangilia wa
habari unavokuwa kabla ya gazeti kuchapishwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri
huyo katika kampuni ya TSN jana Jijini Dar es Salaam
|
 |
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiangalia mashine ya
kuchapishia magazeti ya Serikali inavyofanya kazi alipofanya ziara katika
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) jana Jijini Dar es Salaam
|
 |
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (watano kushoto) katika picha ya
pamoja na menejimenti ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipofanya ziara
katika kampuni hiyo na kuangali shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo jana
Jijini Dar es Salaam
|
 |
Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba (kushoto) akizungumza na
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) alipofanya
ziara TBC jana Jijini Dar es Salaam
|
 |
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza Mkuu wa
TBC Fm Bw. Othuman Iddy (kushoto) alipotembelea studio za TBC Fm wakati wa
ziara yake TBC jana Jijini Dar es Salaam
|
 |
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akimsikiliza mkuu wa
TBC International Bw. Deogratius Salufu (kulia) alipotembela studio za redio hiyo
jana wakati wa ziara yake katika Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Jijini
Dar es Salaam
|
 |
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akiwa katika meza ya
kusomea taarifa ya habari ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jana wakati
wa ziara yake katika TBC Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayob Rioba
|
 |
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na menejimenti ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jana wakati wa
ziara yake TBC Jijini Dar es Salaam. Wa tatu (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu TBC, Dkt. Ayob Rioba (Picha na Genofeva Matemu - WHUSM)
|
COMMENTS