UBALOZI WA USWIDI (SWEDEN) WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 36 KWA UMOJA WA MATAIFA
HomeJamii

UBALOZI WA USWIDI (SWEDEN) WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 36 KWA UMOJA WA MATAIFA

Ubalozi wa Uswidi nchini Tanzania umewekeana saini makubaliano na Umoja wa Mataifa Tanzania ambapo Uswidi imetatoa jumla ya Dola...

WAZIRI LUKUVI KUPEWA TUZO YA UWAJIBIKAJI NA UTENDAJ BORA
MKUU WA WILAYA ILALA MH. SOPHIA MJEMA APONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHUO CHA ST. MARK KATIKA KUELIMISHA JAMII
KAULI YA MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN KTK KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI BUTIAMA



Ubalozi wa Uswidi nchini Tanzania umewekeana saini makubaliano na Umoja wa Mataifa Tanzania ambapo Uswidi imetatoa jumla ya Dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4) kwa shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo. Makubaliano hayo yametiwa saini rasmi na Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez, katika ofisi za Ubalozi wa Uswidi jijini Dar es Salaam.
Mchango wa Uswidi utasaidia jitihada za Umoja wa Mataifa za kuhamasisha ukuaji wa kiuchumi ulio jumuishi na ajira na kuimarisha utawala wa kidemokrasi, haki za binadamu na usawa wa jinsia. Mchango huo pia utasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa na kuondoa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Akifafanua utayari wa dhati wa Uswidi katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania, Balozi Rangnitt alieleza kwamba Uswidi imechagua kusaidia shughuli za Umoja wa Mataifa zinazoakisi malengo ya maendeleo ya nchi katika nyanja za haki za wanawake, utawala wa demokrasia na ukuaji wa uchumi.
Shughuli hizo ni zile zinazomnufaisha kila mmoja katika kipindi ambacho Tanzania inalenga kuwa na uchumi wa kipato cha kati. “Kwa kupitisha sehemu ya msaada wetu kupitia Mfuko wa Umoja wa Mataifa chini ya Mpango wa Kufanya Kazi Pamoja, tunashiriki kikamilifu katika kusaidia ufikiwaji wa malengo ya maendeleo ya Tanzania. Vilevile, tunatambua bayana kabisa na kuthamini wajibu uliokubaliwa kuwa ndio wa Umoja wa Mataifa katika kuleta maendeleo endelevu.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutiliana saini makubaliano ya Dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4) kwa shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo kupitia mashirika ya Umoja wa mataifa kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za ubalozi huo jijini Dar es Salaam., Kushoto ni Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt.
Kwa msaada huu, tunawezesha uchukuaji hatua unaoendana na sera ya nje inayozingatia haki za wanawake ya Uswidi na pia jitihada zinazolenga, miongoni mwa mambo mengine, ajira yenye hadhi na haki za watoto. Hii inadhihirisha mwendelezo wa uhusiano wa karibu na Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania wenye lengo la kuleta maendeleo yenye usawa na jumuishi zaidi,” alisema Balozi.
Akisisitiza utayari wa kuendelea kuisaidia Tanzania na Umoja wa Mataifa, Balozi alitumia fursa hiyo kuthibitisha kuyapokea kwa moyo mmoja mageuzi ya Mfumo wa UN chini ya Mpango wa Kufanya Kazi Pamoja na kutambua njia fungamanifu zinazotumika na thamani inayopatikana kutokana na mchango wa mashirika ya UN katika lengo moja kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania, washirika wa kijamii na vyama vya kiraia.
Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla hiyo fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ya Dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4) kwa shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Rodriguez alitoa shukrani kwa serikali na watu wa Uswidi kwa msaada wao endelevu akiipongeza Uswidi kwa kuwa mshirika wa maendeleo asiyeyumba katika shughuli za Umoja wa Mataifa Moja na pia kwa Tanzania.
“Uswidi imekuwa mshirika wa kuaminika wa Tanzania na Umoja wa Mataifa kwa miongo mingi. Kwa kulenga wale walio wanyonge kabisa katika jamii hii, rasilimali hii itatoa mchango muhimu sana katika kushughulikia mahitaji ya wale ‘walio chini sana’ kama inavyoelekezwa katika Malengo ya Ulimwengu,” alisema.“Mchango huu utauwezesha Umoja wa Mataifa kuweza kufanya kazi katika masuala mapana mengi kama vile kuhamasisha fursa za ajira zenye hadhi kwa Watanzania maskini, kuendeleza kanuni za utawala bora, na nafasi ya uongozi wa wanawake katika masuala ya siasa na vilevile kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,” aliongeza.
Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akikabidhi hati za makubaliano kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4) zilizotolewa na Serikali ya Uswidi kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo kupita mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez (kulia) wakitiliana saini makubaliano ya dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4) kwa shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Uswidi jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt wakibadilishana hati za akubaliano ya Dola za Marekani milioni 36 (takribani Shilingi bilioni 80.4) zilizotolewa na Serikali ya Uswidi kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Uswidi nchini Tanzania, Mh. Katarina Rangnitt wakionyesha hati hizo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutiliana saini makubaliano hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Mary Kawar akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini wa makubaliano hayo iliyofanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa Uswidi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Natalie Boucly akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati hafla fupi ya utiaji saini wa makubaliano hayo iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa Uswidi jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini watakaopata mgao huo kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika miaka minne ijayo kupitia mashirika hayo nchini Tanzania.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UBALOZI WA USWIDI (SWEDEN) WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 36 KWA UMOJA WA MATAIFA
UBALOZI WA USWIDI (SWEDEN) WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 36 KWA UMOJA WA MATAIFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEhjXz2j3j8nISECu_dpWGQH_Pl0WTOK6qo1tt3YVW5QcW8F2GwhAXkE_s0d68rHUTGPdsGis_mTJGiMllICZtSQ4S1EqLI1InCK6F6yCWcbE1oOFX07MW2ldbYUQJVCz6MMpDTsaNvHtkWI6TJg4P5G4v7_0ESycqYr1yIR42rMDZib=s0-d-e1-ft
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEhjXz2j3j8nISECu_dpWGQH_Pl0WTOK6qo1tt3YVW5QcW8F2GwhAXkE_s0d68rHUTGPdsGis_mTJGiMllICZtSQ4S1EqLI1InCK6F6yCWcbE1oOFX07MW2ldbYUQJVCz6MMpDTsaNvHtkWI6TJg4P5G4v7_0ESycqYr1yIR42rMDZib=s72-c-d-e1-ft
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/ubalozi-wa-uswidi-sweden-watoa-dola-za.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/ubalozi-wa-uswidi-sweden-watoa-dola-za.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy