“TATIZO LA MSINGI LA MGOGORO WALOLIONDO LITATATULIWA MEZANI”- DKT. KIGWANGALLA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka viongozi wa Serikali na wale wenye upande wa mgogoro wa pori tengefu l...




Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka viongozi wa Serikali na wale wenye upande wa mgogoro wa pori tengefu la Loliondo kukaa chini ili kupata ufumbuzi wa suala hilo lililochukua karibu miaka zaidi ya 20 sasa huku akitoa tamko la kusitisha operesheni zote zilizokuwa zikiendelea katika suala hilo.

Waziri Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo kwenye mkutano wa wazi jioni ya jana Oktoba 26,2017 wakati akizungumza mamia ya wananchi wa Loliondo wakiwemo wale wenye mgogoro na pori hilo.

“Kuanzia leo, mimi kama Waziri wa Maliasili na Utalii, nina waahidi kufanya uhifadhi endelevu, kukaa na wananchi kuhifadhi. Hivyo nawaomba viongozi wa Serikali na wananchi kwenye mgogoro huu sasa kufikia mwisho na kukaa meza moja.

Mgogoro utatatuliwa kwa kukaa mezani. Kwa pande zote mbili sasa kuja na jibu moja juu ya kusitisha mgogoro huu. Hatutaki tumuone Mkuu wa Wilaya mbaya ama Mkurugenzi wake ama wahifadhi wabaya au Waziri wa Maliasili  bali, sote tuwe kitu kimoja katika meza ya majadiliano na kufikia mwisho” alieleza Dk. Kigwangalla.
Ameongeza kuwa:
“Tutasimamia kushirikiana na nyie. Lakini hatutokubalana na watu miongoni mwetu wa watu ambao wataivunja sheria kwa makusudi. Kwa msingi huo, napenda kutamka kuwa, nasitisha operesheni iliyokuwa ikiendelea Loliondo ile ya kukamata wafugaji na kuwatesa ama vitendo vingine vibaya.
Pili naagiza watalaam wa maji, wakae na watalaam wa hifadhi washirikiane na serikali ya kijiji wawaruhusu wafugaji kunywesha mifugo yao.

Pia naagiza kwa Wahifadhi na Kamati ya Ulinzi na Usalama, mifugo yote ambayo imekamatwa na mamlaka ambayo ipo chini ya Wizara ambayo nasimamia mimi ile yote ambayo haijahukumiwa na mamlaka za kisheria iachiwe huru kwa wenyewe  kwa  mifugo ambayo itabaki chini ya idara iliyopo kwenye wizara yangu ni ile yenye migogoro ya usuluhishi tu” alieleza Dkt.Kigwangalla.

Waziri Dkt. yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya siku sita ambapo awali alianza kutembelea Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) mjini Arusha, na baadae Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo pia aliweza kukutana na jamii ya wafugaji wanaoishi kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kutatua migogoro kati yao na wahifadhi wa Ngorongoro.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongea na wananchi wakati wa ziara yake Mkoani Arusha.



(Picha kwa hisani ya WMU)


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: “TATIZO LA MSINGI LA MGOGORO WALOLIONDO LITATATULIWA MEZANI”- DKT. KIGWANGALLA
“TATIZO LA MSINGI LA MGOGORO WALOLIONDO LITATATULIWA MEZANI”- DKT. KIGWANGALLA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhc5hfAvZLRu-CtqT4LskBIMQlKevjHQIHTE56_pKfKx0qrWCXmwanCwihCcBWixxu_2xWwT6RkmBHVdZbVwBa1FVAgPDmx0F0MYGP_dTAArSrEwSj9bgp3xy_pQEIQv7AfZYDpWJYWfBA/s640/_J8A9757.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhc5hfAvZLRu-CtqT4LskBIMQlKevjHQIHTE56_pKfKx0qrWCXmwanCwihCcBWixxu_2xWwT6RkmBHVdZbVwBa1FVAgPDmx0F0MYGP_dTAArSrEwSj9bgp3xy_pQEIQv7AfZYDpWJYWfBA/s72-c/_J8A9757.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/tatizo-la-msingi-la-mgogoro-waloliondo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/tatizo-la-msingi-la-mgogoro-waloliondo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy