TAASISI YA' ROOM TO READ ' YAMPA TUNZO MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI
HomeJamii

TAASISI YA' ROOM TO READ ' YAMPA TUNZO MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

MKE wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete jana alikabidhiwa tuzo ya heshima kutokana na kutambua jitihada zake za kumlinda na kumte...

POLISI YAAGIZA MAKAMANDA WAKE KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA
SIKU YA WAPENDANAO NINI ASILI YAKE!
WANAHABARI WATAKIWA KUACHA KUAMINI KILA KITU, WASOME




MKE wa Rais wa awamu ya nne mama Salma Kikwete jana alikabidhiwa tuzo ya heshima kutokana na kutambua jitihada zake za kumlinda na kumtetea mtoto wa kike iliyotolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali inayifahamika kwa jina la Room to Read.


Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo Mkurugenzi wa Room To Read Peter Mwakabwale kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Bwawani Kihaba Maili Moja Mkoani Pwani.


Akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka katika shule mbalimbali za mkoa wa Pwani mama Kikwete amezitaka Hamlashari kutenga bajeti ya kujenga mabweni katika shule kwa ajili ya wanafunzi wakike sanjari na kujenga maabara na vyumba vya madarasa ili kuweza kuwarahisishia wanafunzi hususani wasichana ili waweze kujifunza bila kikwazo chochote na kufaulu vema masomo yao.

Aidha Mama Salma Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo yameadhimishwa kimkoa Kibaha Mkoani Pwani.


Mama Salma Kikwete amesema kuwa Mkoa wa Pwani unashika nafasi ya kumi kitaifa kwa mimba huku sababu mojawapo ni ukosefu wa mabweni ya wasichana hali inayopelekea wasome shule za kutwa na kukutana na vishawishi wawapo njiani kuelekea ama kurudi shule.


Maadhimisho hayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room to Read linaloendesha mradi wa Elimu kwa Wasichana katika mkoa wa Pwani na kuzihusisha Wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Kibaha ambapo wamekuwa wakitoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana lakini pia kuwasaidia gharama za mahitaji ya shule pamoja na karo kwa familia zisizo na uwezo wa kifedha

Siku ya kumuenzi mtoto wa kike huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 11 kufuatia maazimio ya malengo endelevu ya Umoja wa mataifa , viongozi wa nchi mbalimbali duniani walikubaliana na kuyapitisha huku miongoni mwa malengo matano mojawapo kuhakikisha tunafikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wasichana na wanawake wote duniani ifikapo mwaka 2030.

Wahamasishaji wa Mradi wa Elimu kwa wasichana Room to Read wakionesha kazi wanazozifanya katika maadhimisho ya mtoto wa Kike duniani October 11 mkoani Pwani -kibaha
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAASISI YA' ROOM TO READ ' YAMPA TUNZO MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI
TAASISI YA' ROOM TO READ ' YAMPA TUNZO MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWlbsTt7XJwSZUQI5bAq85PIh4agum9ETBoWPCDVFBE62yr5y0OEuSXPd7C2XGAdQM6MQDKa8iGFESzD0mMoXcJvgrVvMnacAS8ID-4CL7yokpqUgvKHZKlVNj0X_hRdFEAW1XggqbjGKT/s640/WhatsApp+Image+2017-10-12+at+15.38.36.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWlbsTt7XJwSZUQI5bAq85PIh4agum9ETBoWPCDVFBE62yr5y0OEuSXPd7C2XGAdQM6MQDKa8iGFESzD0mMoXcJvgrVvMnacAS8ID-4CL7yokpqUgvKHZKlVNj0X_hRdFEAW1XggqbjGKT/s72-c/WhatsApp+Image+2017-10-12+at+15.38.36.jpeg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/taasisi-ya-room-to-read-yampa-tunzo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/taasisi-ya-room-to-read-yampa-tunzo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy