POLISI YAAGIZA MAKAMANDA WAKE KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA
HomeJamii

POLISI YAAGIZA MAKAMANDA WAKE KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI JESHI LA POLISI TANZANIA Anuani ya Simu “ MKUUPOLISI”                       ...

WANAWAKE KANISA LA PENTEKOSTE WAOMBA AMANI ILIYOPO NCHINI IDUMISHWE
VIJANA DAR ES SALAAM WAANZISHA KLABU ZA MABADILIKO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI
KARIAKOO FAMILY DEVELOPMENT FOUNDATION CHAPATA UONGOZI MPYA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA



Anuani ya Simu “ MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                               Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                               Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                     S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                DAR ES SALAAM.

          

                                                                                                                      14/02/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika kuhakikisha kuwa biashara haramu ya dawa za kulevya inakomeshwa hapa nchini na kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya, Jeshi la Polisi nchini limetoa maelekezo kwa  Makamanda wa Polisi katika mikoa yote kuongeza nguvu za Oparesheni katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kuwakamata wanaotumia, wanaouza na wanaosafirisha.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini limewaagiza Makamanda wote pindi wanapoendesha oparesheni dhidi ya dawa za kulevya kutokuangalia sura ya mtu, cheo, wadhifa wala nafasi aliyonayo katika jamii.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini linakemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaokusanyika katika vituo vya Polisi pindi baadhi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali wanapotakiwa kufika kwenye vituo hivyo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma wanazokabiliwa nazo. Ni marufuku kwa mtu ama kikundi chochote kukusanyika katika kituo cha Polisi bila ya kuwa na sababu ya msingi na watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Jeshi la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu zikiwemo za watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na taarifa hizo zitafanyiwa kazi kwa siri ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa katika hali ya usalama.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba-ACP,
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
MAKAO MAKUU YA POLISI.
  
Advera John Bulimba-ACP, Msemaji wa Jeshi la Polisi (Picha na Robert Okanda Blogspots)

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: POLISI YAAGIZA MAKAMANDA WAKE KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA
POLISI YAAGIZA MAKAMANDA WAKE KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA
https://lh4.googleusercontent.com/2YWpQEOFSKXg9wVwotouZIZODNYW2huEYkslbMEBvQ-v4jueHh5gV8TxRjY0WN1ELX632frmqEUleQUzoLQhgHAburbisRsTLqqaozZJB0rOp9HDD_uDj5c1bEwz1PqvrAvnEMoF3N41DxKtEg
https://lh4.googleusercontent.com/2YWpQEOFSKXg9wVwotouZIZODNYW2huEYkslbMEBvQ-v4jueHh5gV8TxRjY0WN1ELX632frmqEUleQUzoLQhgHAburbisRsTLqqaozZJB0rOp9HDD_uDj5c1bEwz1PqvrAvnEMoF3N41DxKtEg=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/polisi-yaagiza-makamanda-wake-kuongeza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/polisi-yaagiza-makamanda-wake-kuongeza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy