NAMBA MAALUMU YAZINDULIWA KUCHANGIA MFUKO WA UKIMWI
HomeJamii

NAMBA MAALUMU YAZINDULIWA KUCHANGIA MFUKO WA UKIMWI

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akikata ut...

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO AAGIZA KUANZA UJENZI WA MADARASA MANNE NA VYOO VYA SHULE YA SEKONDARI MBURAHATI
UJUMBE WA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUHUSU MADINI
SPIKA NDUGAI ATEMBELEA BUNGE LA KENYA




 Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa namba
maalumu ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.  Wanaoshuhudia kulia kwake ni Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu na  Mwenyekiti wa Bodi ya
mfuko huo, Godfrey Simbeye. Kushoto kwa Mhagama ni Waziri wa TAMISEMI, Suleiman
Jafo na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Khamis Mwinyimvua.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati)
akifurahia pamoja na viongozi wenzake  mara
baada ya uzinduzi huo.
 Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 660 Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu.


 Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo akimkabidhi hundi ya sh. milioni
200 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera ( kulia) kwa ajili ya ujenzi wa
kituo cha afya Mererani. 
 Mwenyekiti
wa bodi wa mfuko, Godfrey Simbeye akizungumza kabla ya uzinduzi wa namba hizo.
 Mkurugenzi
Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko akizungumza kwenye tukio hilo.
 Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama akitoa hotuba katika tukio hilo.
 Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akisisitiza jambo baada ya kukabidhiwa
hundi yake.
 Washiriki
wakifuatilia mkutano huo.
 Mawaziri
wakiangalia namna ya kutuma fedha kwa kutumia namba  0684909090 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa
udhamini wa kudhibiti Ukimwi. Aliyesimama ni Mkuu wa kitengo cha sheria wa
TACAIDS, Elizabeth Kaganda.
 Waziri
Mhagama (katikati) akiwa katika picha na viongozi wengine.
 Mawaziri wakiagana mara baada ya kumaliza uzinduzi wa tukio hilo.

(Picha na Philemon Solomon)
.....


Na Julian Msacky-Nchi yangu Blog.



TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), imezindua rasmi
namba maalumu ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.






Uzinduzi huo umefanyika Dar es Salaam Oktoba 21, 2017 na kuzinduliwa
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Jenista Mhagama.





Mhagama alitaja namba ya uchangiaji wa mfuko huo kuwa ni
0684909090 na kwamba kila mwananchi anahimizwa kuchangia ili fedha
itakayopatikana isaidie watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi. 






"Leo ni siku maalumu kwa nchi yetu...inaonesha
tumeanza kujitegemea kupitia mfuko huu wa udhamini katika mapambano dhidi ya
VVU na Ukimwi," alisema.




Waziri alisema mfuko huo umeanzishwa kwa Sheria Namba 6 ya Mwaka
2015 na utakuwa unachangiwa na Watanzania wenyewe.






"Huu ni mfuko wa umma na tunabeba jukumu hilo kama
Serikali na lengo kuu ni kuwahudumia Watu wenye maambukizi,"
alibainisha.






Alisema fedha za mfuko huo zitatumika kununua dawa za
septrine ambazo ni maalumu kwa ajili ya kufubaza Virusi Vya Ukimwi na
zitatolewa bure.






Mhagama alisema takwimu zinaonesha kuna Watanzania milioni
1.4 wanaoishi na VVU na watu 48,000 huambukizwa virusi hivyo kila mwaka nchini.






"Kati ya WAVIU milioni 1.4 wanaotumia dawa ni laki
8, Watanzania kati ya laki 4 hadi 5 hawatumii dawa, hivyo tupunguze utegemezi
angalau kwa asilimia 40 ili kudhibiti Ukimwi," alifafanua.






Pamoja na hali kuwa hivyo, Waziri alisema asilimia 94.7 ya
Watanzania hawana VVU na Ukimwi na wanahitaji kulindwa ili waendelee
kubaki salama.






Alisema kulingana na Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti
Ukimwi (2013/14-2017/18) uliothaminishwa, mahitaji ya taifa ya kugharimia
mwitikio wa Ukimwi katika kipindi cha miaka mitano yanakadiriwa kufikia sh.
trilioni 6.





"Asilimia 93 ya fedha hizi zinatarajiwa kutoka kwa
wafadhili na asilimia 7 kutoka vyanzo vya ndani. Sehemu kubwa asilimia 56 ya
fedha zote katika miaka hiyo ni kwa ajili ya kununua dawa," alisisitiza.






Katika hatua nyingine, Mhagama alikabidhi hundi ya sh.
milioni 660 kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu kwa ajili ya kununua dawa aina ya cotrimoxazole za watu wanaoishi
na VVU.






Pia alikabidhi hundi ya sh. milioni 200 kwa Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Dk Joel Bendera ili kujenga kituo cha afya Mererani ikiwa ni kuunga
mkono ahadi ya Rais John Magufuli kusaidia ujenzi wa kituo hicho.






Viongozi wengine walioshiriki tukio hilo la uzinduzi ni
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, DK Leonard Maboko na Mwenyekiti wa bodi wa mfuko
huo, Godfrey Simbeye.





Habari
hii imeandaliwa na blog ya NCHI YANGU. Simu 0718981221

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAMBA MAALUMU YAZINDULIWA KUCHANGIA MFUKO WA UKIMWI
NAMBA MAALUMU YAZINDULIWA KUCHANGIA MFUKO WA UKIMWI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXECXq2hOh_RT0QNNHlaAxWtbG0hpWsOtGNF7cvElUsm0LLuDCWY6ScY2cM2olmaUt9yJXJhe6vKOd1lX15VSsNGzFtEIjm_Aa-cZU6hh0g5MivMXB0QPxYZeQSs5_68N8GyUj-0BvUCo/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXECXq2hOh_RT0QNNHlaAxWtbG0hpWsOtGNF7cvElUsm0LLuDCWY6ScY2cM2olmaUt9yJXJhe6vKOd1lX15VSsNGzFtEIjm_Aa-cZU6hh0g5MivMXB0QPxYZeQSs5_68N8GyUj-0BvUCo/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/namba-maalumu-yazinduliwa-kuchangia.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/namba-maalumu-yazinduliwa-kuchangia.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy