MZEE RUKSA AWAASA WAZEE WENZAKE NA JAMII KWA UJUMLA
HomeJamii

MZEE RUKSA AWAASA WAZEE WENZAKE NA JAMII KWA UJUMLA

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, "Mzee Rukhsa" akizungumza na wazee wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Du...

WATOTO WENYE SARATANI WALA KRISMASS NA WAFANYAKAZI WA SOUTHERN SUN HOTEL
MAKAMU WA RAIS, MHE SAMIA SULUHU AHAMIA DODOMA RASMI
WALIODANGANYA RUZUKU YA UCHIMBAJI WATAKIWA KUREJESHA







Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, "Mzee Rukhsa" akizungumza na wazee wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017 .


NA WAMJW
Vijana nchini wameshauriwa kujitolea na kuwatunza wazee katika maeneo yao ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa maendeleo yao na taifa.
Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wazee katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kila Oktoba Mosi ya kila mwaka.
Mhe. Mwinyi amesema kuwa jukumu la kuwatunza na kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii pia ina nafasi yake katika kuwatunza wazee hasa Vijana.
Mhe. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali imejitaidi sana kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za Afya na kuwatunza wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali ya wazee nchini.
“Niwaombe vijana mtutunze sisi wazee kwani na sisi tulikuwa vijana kama ninyi na mkiweka utamaduni huu utawasaidia na ninyi mkiwa wazee hapo baadae” alisema Mhe. Mwinyi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, MAendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Mstaafu Mhe. Mwinyi kuwa Serikali itaendelea kuwatunza wazee nchini na kuhakikisha wanapata hudumu zote muhimu.
“Nikuhakikishie Mhe. Mwinyi kuwa tutaendelea kuwatunza wazee kwa kuwapatia huduma muhimu hasa huduma za Afya” alisema Mhe. Ummy.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini Mzee Sebastian Bulegi amemuomba Mhe. Mwinyi kufikisha shukurani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa moyo wake wa kuwajali wazee nchini.
“Mhe. Mwinyi naomba utufikishie shukurani zetu kwa Mhe.Rais Magufuli kwa kutujali wazee hasa kwa kutatua changamoto zetu zinazotukabili” alisema Mzee Sebastian.
Siku ya Wazee Duniani huadhimishwa Oktoba Mosi kila mwaka kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa linalozitaka nchi wanachama kutenga siku maalumu ya kutafakari mchango wa Wazee katika maendeleo ya jamii na kuwaenzi ili wawe na maisha bora na yenye matumaini na Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “ Kuelekea uchumi wa Viwanda:Tuthamini Mchango, Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa maendeleo ya Taifa”.




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu za Mkoa kwa Mgeni Rasmi wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwapungia mkono wazee wakati wakiingia kwa maandamano kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 kwa Mgeni wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.


Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini Mzee Sebastian Bulegi akisoma hotuba kwa niaba ya Wazee nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017



Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi (hayupo Pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.



Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi (hayupo Pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na wazee katika moja ya banda la Maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MZEE RUKSA AWAASA WAZEE WENZAKE NA JAMII KWA UJUMLA
MZEE RUKSA AWAASA WAZEE WENZAKE NA JAMII KWA UJUMLA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGQWWt190M5P7qPfd_yoL5HQaEsezt61igVXRJqyPUkGUfVdugZw58HFsXiGkqU0jlKVsYxfsB7fmPgXli-cpclPY_a6FEQpdpb5FWKpuVKg_lVPPqlA8k1ELrf39E_R-Ec9QyMW4sXFd_/s640/Pix+5.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGQWWt190M5P7qPfd_yoL5HQaEsezt61igVXRJqyPUkGUfVdugZw58HFsXiGkqU0jlKVsYxfsB7fmPgXli-cpclPY_a6FEQpdpb5FWKpuVKg_lVPPqlA8k1ELrf39E_R-Ec9QyMW4sXFd_/s72-c/Pix+5.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/mzee-ruksa-awaasa-wazee-wenzake-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/mzee-ruksa-awaasa-wazee-wenzake-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy