MASHINDANO YA WANAFUNZI WA SEKONDARI KWA MASWALA YA KODI YAFANA DAR ES SALAAM
HomeJamii

MASHINDANO YA WANAFUNZI WA SEKONDARI KWA MASWALA YA KODI YAFANA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu. Mamlaka ya mapato nchini (TRA) iliendesha na kudhamini shindano la shule za sekondari za Mkoa wa Dar es...

SERIKALI YATENGA BILIONI 30 KAMA FIDIA KWA WAKAZI WA KIPUNGUNI”-MHE.NGONYANI
BALOZI FATMA AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO NCHINI QATAR
MAKAMU WA RAIS ALIVYOONGOZA WANANCHI WA ARUSHA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI, WALIMU NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VICENT










Na Mwandishi Wetu.
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) iliendesha na kudhamini shindano la shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani jijini humo. Mashindano hayo yaliyoshirikisha shule mbalimbali za Dar es salaam na Pwani lilipambwa na maigizo ya maswala ya kodi ambapo mgeni Rasmi alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere.

Shule ya Sekodari Misitu iliyotia fora katika ufunguzi wa mashindano hayo ulimvutia mgeni rasmi na kudhamiria kushiriki mashindano hayo mwanzo hadi mwisho ambapo alipata fursa ya kujionea na kufurahia vipaji vya wanafunzi waliondaliwa vyema kuwa mabalozi wa maswala ya kodi katika nyanja mbalimbali kwa sasa na siku zijazo. 

Baada ya kufungua mashindano hayo yaliyonogeshwa na wanafunzi wenye vipaji mbalimbali vya kuwasilisha mada hatimaye shule ya sekondari Tumbi iliibuka kidedea na kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Kombe, Luninga ya Kisasa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti. 

Shule ya Sekondari Minaki ilichukuwa nafasi ya pili ikijinyakulia pia Kikombe, Komputa, Printa, Saa ya ukutani na cheti huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Shule ya Sekondari Maarifa ambayo kadhalika ilipata Kikombe, Komputa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti.

Hadija Jumanne Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Misitu aliibuka Muwasilishaji mada bora na kujinyakulia Komputa mpakato, Saa ya Ukutani, Kikombe cha chai chenye chapa ya TRA. 

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere baada ya kukunwa na uzuri wa mashindano hayo aliahidi kuyaboresha zaidi mwakani ili kuwapa motisha zaidi wanafunzi na walimu wao kujiandaa vyema na kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kodi ambayo ndio mhimili muhimu wa kuboresha huduma za jamii na kuleta maendeleo kwa nchi. 

Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio ya mashindano hayo. 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili  kulia) akiwasili ukumbi wa Chuo cha Kodi (ITA) kuhudhuria mashindano ya Kodi kwa Shule za Sekondari za Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani yaliyoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kulia) ni    Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho.  
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Hadija Jumanne Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Misitu baada ya kuibuka mwanafuzi bora katika uwasilishaji wa mada ihusuyo kodi ya ongezeko la thamani (VAT), wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)



Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Mwalimu shule ya Sekodanri Jangwani zawadi ya kikombe baada wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo (wa tatu kulia) na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati.  

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiwa wamembeba mwalimu wao Boniface Mulambo baada yakukadidhiwa zawadi ya Kikombe na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere kwa kuwaandaa vyema wanafunzi wake walioshiriki mashindano hayo. 

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MASHINDANO YA WANAFUNZI WA SEKONDARI KWA MASWALA YA KODI YAFANA DAR ES SALAAM
MASHINDANO YA WANAFUNZI WA SEKONDARI KWA MASWALA YA KODI YAFANA DAR ES SALAAM
https://i.ytimg.com/vi/ocm5KGlxJ9o/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/ocm5KGlxJ9o/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/mashindano-ya-wanafunzi-wa-sekondari_23.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/mashindano-ya-wanafunzi-wa-sekondari_23.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy