MAKAMU WA RAIS ALIVYOONGOZA WANANCHI WA ARUSHA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI, WALIMU NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VICENT
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha Mei 8, 2017
HomeJamii

MAKAMU WA RAIS ALIVYOONGOZA WANANCHI WA ARUSHA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI, WALIMU NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VICENT

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanafun...

TANZANIA YASHINDA TUZO YA TEKNOLOJIA KATIKA MKUTANO WA DUNIA WA SERIKALI (WORLD GOVERNMENT SUMMIT 2018)
MSD YATUNUKIWA ITHIBATI YA JUU YA UBORA
WAZIRI MAHIGA AFANYA MAZUNGUMZO NA WABUNGE WA EALA







Jeshi la Wananchi(JWTZ) wakiingiza miili ndani ya uwanja kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliofika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili hiyo.

Miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent ikiwa katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuombewa pamoja na kuagwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwafariji ndugu na jamaa wa marehemu waliofika kuaga miili ya ndugu zao katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Kiserikali na chama wakiwa kwenye uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vicent.
Wanafunzi wa shule ya Lucky Visent wakiwa kwenye majonzi wakati wa kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vicent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakiwa  katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vicent waliofariki kwenye ajali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan tarehe 8-May-2017 ameongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Arusha na Mikoa ya Jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili na pamoja na Dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha waliopata ajali katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Katika hotuba yake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika tukio la kuaga miili hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia waombolezaji kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na chenye majonzi mazito kwa kuondokewa na wapendwa wao.

Amehimiza wananchi kote nchini kuungana katika msiba uliotokea kwa kuwafiriji wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali peponi.

Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi nchini,walimu, wazazi na walezi wawe makini katika kuhakikisha kuwa sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua stahiki za kulinda watoto hasa wanapotumia vyombo vya moto kwenye shughuli zao za kimasomo.

Amesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha matukio ya ajali ambayo yanaweza kuzuilika kote nchini.

Makamu wa Rais amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani na waache kutumia pombe na dawa za kulevya ili kuepukana na ajali ambazo zinagharimu maisha ya wananchi.

Makamu wa Rais pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.

Katika kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Jijini Arusha, Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amewakilishwa na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Fred Matiang’i.

Ibada na Dua ya kuaga miili hiyo, imehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali ikiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohammed Aboud,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene, Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Viongozi wa vyama vya siasa na Viongozi wa Dini.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS ALIVYOONGOZA WANANCHI WA ARUSHA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI, WALIMU NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VICENT
MAKAMU WA RAIS ALIVYOONGOZA WANANCHI WA ARUSHA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI, WALIMU NA DEREVA WA SHULE YA LUCKY VICENT
https://i.ytimg.com/vi/WZ9ZgT-jvMc/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/WZ9ZgT-jvMc/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/05/makamu-wa-raisi-alivyoongoza-wananchi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/makamu-wa-raisi-alivyoongoza-wananchi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy