Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akishuka katika Meli ya Mfalme wa Oman mara baada ya kumalizika k...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akishuka katika Meli ya Mfalme wa Oman mara baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika leo ndani ya Meli hiyo.Meli hiyo iliwasili jana jijini Dar es Salaam ikiwa na ujumbe wa watu 350 wakiongozwa na Mawaziri wa Mafuta na Gesi, Uwekezaji, na Waziri wa Utalii kutoka Serikali ya Oman.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na ujumbe kutoka Oman alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika leo ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman iliyowasili jijini Dar es Salaam jana ikiwa na ujumbe wa watu 350 wakiongozwa na Mawaziri wa Mafuta na Gesi, Uwekezaji na Utalii kutoka Serikali ya Oman. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akisalimiana baadhi ya ujumbe na ujumbe kutoka Oman mara baada ya hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika leo ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman iliyowasili jijini Dar es Salaam jana ikiwa na ujumbe wa watu 350 wakiongozwa na Mawaziri wa Mafuta na Gesi, Uwekezaji, na Waziri wa Utalii kutoka Serikali ya Oman.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akitazama baadhi ya picha za historia ya Oman zilizohifadhiwa katika makumbusho iliyopo ndani ya meli ya Mfalme wa Oman katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika leo ndani ya Meli hiyo iliyowasili jijini Dar es Salaam jana ikiwa na ujumbe wa watu 350 wakiongozwa na Mawaziri wa Mafuta na Gesi, Uwekezaji, na Waziri wa Utalii kutoka Serikali ya Oman. Kulia ni Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohammed Bin Hamad Al Rumhy

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Dkt. Hamis Kigwangalla(kulia) akimsikiliza Waziri wa masula ya Utalii kutoka Oman Maitha Saif Majid Al- Mahrouqi, kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Serikali ya Oman Dkt. Mohammed Bin Hamad Al Rumhy ambaye ni kiongozi ujumbe kutoka Oman mara baada ya hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika leo ndani ya Meli ya Mfalme wa Oman iliyowasili jijini Dar es Salaam jana ikiwa na ujumbe wa watu 350 wakiongozwa na Mawaziri wa Mafuta na Gesi, Uwekezaji, na Waziri wa Utalii kutoka Serikali ya Oman. (PICHA NA: FRANK SHIJA – MAELEZO)
COMMENTS