Na Jeshi la Polisi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Maofisa na Askari Polisi kote nchini kushiriki michezo ili ...
Na Jeshi la
Polisi
Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Maofisa na Askari Polisi kote nchini
kushiriki michezo ili kujenga Afya,ukakamavu na urafiki baina ya wenyewe kwa
wenyewe na raia.
IGP Sirro
ameyasema hayo jijini Dae es Salaam wakati hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji
wa TAEKWONDO waliofanya vizuri katika michezo ya Taekwondo Pumsae (kucheza
Kata), Taekwondo Gyeokpa (kuvunja kibao kwa kuruka Juu) na Taekwondo Gyeorugi
(Mapigano) iliyomalizika hivi karibuni ambapo timu ya Polisi iliibuka na ushindi
wa kwanza katika timu 17 zilizoshiriki.
Sirro alisema
Jeshi la Polisi litaendelea kutilia mkazo michezo ya aina mbalimbali na
atahakikisha Askari na Maofisa wanapata fursa ya kushiriki michezo kwakuwa
kwakufanya hivyo kutasaidia pia kulitangaza Jeshi la Polisi na kujenga
mahusiano na jamii.
"Hakikisheni
hamrudi nyuma,tutawapa sapoti ya kila namna ili tusiwe wasindikizaji bali
tuweze kutoa ushindani na kufanya vyema na ni jambo linalowezekana kwa kuwa ari
na morali ipo"Alisema Sirro.
Kwa Upande wake
Mkuu wa Michezo wa Jeshi la Polisi,Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philip
Kalangi alisema ushindi wa timu hiyo ni chachu katika kujiandaa na michezo ya
majeshi ya EAPCCO itakayofanyika hapa nchini mwakani ambapo Tanzania itakuwa
mwenyeji.
mashindano
hayo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Jamhuri ya korea ukishirikiana na Chama cha
Walimu wa Taekwondo kutoka korea (Korean Taekwondo Masters Association) ambayo
ni mashindano ya Taekwondo ya kitaifa yaliyofanyika tarehe 21/10/2017 ambayo
yalishilikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka
nchi nzima ambavyo ni Makongo Juu, Kariakoo,Shark TKD,Twiga Triple A,HTC
DSM, KILI, Vingunguti,Arusha Morden,TCC,AICC,UAUT pamoja na vilabu vya Polisi
ambavyo ni DPA, MPA na ZPA
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na askari wa jeshi hilo wanaounda timu ya Taekwondo ambao walishiriki na kujinyakulia medali mbalimbali katika mashindano ya Taekwondo yaliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association) yaliyoshirikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka nchi nzima.
|
COMMENTS