DC MTATURU ALAMBA DUME ASHINDA UJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA
HomeSiasa

DC MTATURU ALAMBA DUME ASHINDA UJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akionyesha namba yake ya ...

SHAKA AINGIA PEMBA KWA KISHINDO
CCM YAHITIMISHA MAFUNZO ELEKEZI YA SIKU MBILI KWA MAKATIBU WA CCM MIKOA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI MJINI DODOMA
MBUNGE WA UBUNGO SAED KUBENEA AKAGUA BARABARA YA MAKOKA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI MMOJA MMOJA
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akionyesha namba yake ya ushiriki ambayo ni namba 6 mara baada ya kuzungumza mbele ya wajumbe kuwaomba kura 

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitumia haki yake ya kikatiba ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya CCM

Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi wakifatilia mkutano huo uliomalizika kwa salama na amani
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa kwa kishindo. katika nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Katikati) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kushoto) na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo Ndg Hassan Tati wakifatilia mkutano Mkuu wa CCM

Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa kwa kishindo

Baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa wakifatilia mkutano huo uliomalizika kwa salama na amani.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa na wagombea wengine wa nafasi hiyo akionyesha namba yake ya ushiriki ambayo ni namba 6 mara baada ya kuzungumza mbele ya wajumbe kuwaomba kura.
  
Na Mathias canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Leo Jumamosi Octoba 7, 2017 amewazidi mbinu za ushawishi washindani wenzake 10 waliokuwa wakiwania nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.

Wajumbe 989 kati ya wajumbe halali waliojiandikisha 1034 wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ikungi wamemuwezesha Mhe Mtaturu kuwa kinara katika matokeo hayo kwa kuungwa mkono kwa kura nyingi.

Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa kauli moja wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.

Mkutano huo ulifanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi  eneo na Kata ya Ikungi na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.

Mjumbe huyo wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Mhe Mtaturu ataungana na wenzake walioshika nafasi ya pili na ya tatu ambao ni Mwanga Ally Juma aliyepata kura 620, na Yunde Celestine Kimu aliyepata kura 612 kuwakilisha Wilaya ya Ikungi katika kikao muhimu cha maamuzi cha CCM Taifa.

Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya kutangazwa mshindi katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Mhe Mtaturu amesifu imani kubwa aliyoonyeshwa na wajumbe wote huku akiwasihi kuonyesha zaidi ushirikiano katika kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.

Aliahidi kutekeleza na kusimamia kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 huku akiwasihi wananchi kwa kauli moja kushirikiana na Viongozi wote wa Chama na serikali hususani kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia wananchi pasina kujali maslahi yake binafsi. 

Mhe Mtaturu aliwasihi wajumbe wote kuwaunga mkono washindi wa nafasi zote za uongozi ndani ya CCM ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika kuwatumikia.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha uchaguzi wa ngazi ya chama na hata serikali kila mwananchi huwa na maono na mtazamo wake kwa kiongozi amtakaye lakini pindi anapochaguliwa kiongozi mmoja ni wazi ni vyema ikawa mwisho wa makundi hayo hivyo kuwa na mshikamano mpya katika uwajibikaji.

Wagombea wengine ambao hawajafanikiwa kuvuka kiunzi katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ni pamoja na Ayubu Heleni Petro, Bollosi Tatu Mohamed, Mghenyi John Mathias, Mghenyi Juma Shabani, Mkhotya Prorice Patrick, Muna abubakar Omary, Siphy Iddy Selemani, na Sunja Mussa Ntandu.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DC MTATURU ALAMBA DUME ASHINDA UJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA
DC MTATURU ALAMBA DUME ASHINDA UJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1CauoPUlfv_oDFTDTY2ae3mUU1mKovAG_14c-bE4KTviB20JRAIPN7xGyv0KGvDlGPP1PqRhmr2v37UthmxfwH6b79hIVLwfESQKUpzzy1sDmnQY6qAr0PFks9gfY27_-mP_ZqXQTZVg/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1CauoPUlfv_oDFTDTY2ae3mUU1mKovAG_14c-bE4KTviB20JRAIPN7xGyv0KGvDlGPP1PqRhmr2v37UthmxfwH6b79hIVLwfESQKUpzzy1sDmnQY6qAr0PFks9gfY27_-mP_ZqXQTZVg/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/dc-mtaturu-alamba-dume-ashinda-ujumbe.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/dc-mtaturu-alamba-dume-ashinda-ujumbe.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy