WAZIRI LUKUVI APOKEA RIPOTI YA MUFTI WA TANZANIA KUHUSU UFISADI ULIOFANYWA KWENYE MILKI YA MAENEO YA WAISLAMU
HomeJamii

WAZIRI LUKUVI APOKEA RIPOTI YA MUFTI WA TANZANIA KUHUSU UFISADI ULIOFANYWA KWENYE MILKI YA MAENEO YA WAISLAMU

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi Ripoti ya Tume...

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA SHWREHE ZA MWAKA MPYA WA KICHINA JIJINI DAR ES SALAAM
KUWENI MACHO NA MATAPELI WA FEDHA ZA M-PESA
TPSC KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA-WAZIRI KAIRUKI




Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi Ripoti ya Tume ya Mufti ofisini kwa Waziri.




Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akimsisitiza kufuatilia kwa makini maeneo yote ya waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikishwa watu kinyume cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais.

Ujumbe wa Tume ya Mufti ukiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi ofisini kwake.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akimsikiliza Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir mara baada ya kupokea Ripoti ya Tume ya Mufti ofisini kwake, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA Mwalimu Salim Abeid na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi baada ya kumkabidhi Ripoti ya Tume ya Mufti.
……………………….
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amekutana na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir pamoja ujumbe wake wa Tume ya Mufti iliyoundwa kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA zinar ejeshwa.
Waziri Lukuvi amepokea ripoti hiyo ikiwa ni kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli la kumtaka Waziri Ardhi afuatilie kwa makini maeneo yote ya waislam yanayomilikiwa na BAKWATA na yaliyomilikiswa watu kinyume cha utaratibu yanatafutiwa ufumbuzi.
Katika ujumbe huu Mufti ameongozana na Kaimu Katibu Mkuu wa BAKWATA Mwalimu Salim Abeid, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Ally Ngeruko, Makamu mwenyekiti wa Tume ya Mufti na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Issa Othman Issa na Katibu wa Tume ya Mufti Alhaj Omary Igge.
Baada ya kukabithi ripoti hii Mufti Sheikh Abubakar Zubeir amemshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kupokea Ujumbe wake wa Tume ya Mufti na kumuomba achunguze na kuchambua kwa makini maeneo yote ya Bakwata yanayohusiana na migogoro ya ardhi.
Tume hii ya Mufti ya Kuhusu urejeshaji wa mali za waislam iliundwa na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir mara baada ya kukukutana Mheshimiwa Rais na kumuomba awasaidie kuhakikisha kwamba mali za waislam zinazomilikiwa na BAKWATA zinarejeshwa BAKWATA.
Mara baada ya kupokea ripoti hii Waziri Lukuvi amemuahidi Mufti Sheikh Abubakar Zubeir kwamba atatekeleza agizo hilo la Mheshimiwa Rais na ataifanya kazi hii katika muda mfupi ujao na kusimamia kikamilifu kwa kufuata sheria.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI LUKUVI APOKEA RIPOTI YA MUFTI WA TANZANIA KUHUSU UFISADI ULIOFANYWA KWENYE MILKI YA MAENEO YA WAISLAMU
WAZIRI LUKUVI APOKEA RIPOTI YA MUFTI WA TANZANIA KUHUSU UFISADI ULIOFANYWA KWENYE MILKI YA MAENEO YA WAISLAMU
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/09/2-29.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/waziri-lukuvi-apokea-ripoti-ya-mufti-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/waziri-lukuvi-apokea-ripoti-ya-mufti-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy