WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA PEACE CORPS WAPATAO 57 WAAPISHWA KUHUDUMU NCHINI KWA MIAKA MIWILI
HomeJamii

WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA PEACE CORPS WAPATAO 57 WAAPISHWA KUHUDUMU NCHINI KWA MIAKA MIWILI

On Thursday, September 21: U.S. Chargé d’Affaires Dr. Inmi Patterson swore in 57 Peace Corps Volunteers to their two years of service i...






On Thursday, September 21: U.S. Chargé d’Affaires Dr. Inmi Patterson swore in 57 Peace Corps Volunteers to their two years of service in Tanzania. The American volunteers will work in the education field in 27 districts. The ceremony was held at the Peace Corps offices in Dar es Salaam and attended by the Permanent Secretary of the Ministry of Education, Science and Technology, Dr. Leonard Akwilapo. Above, volunteers take the oath that was administered by Dr. Patterson. (Photo: courtesy of U.S. Embassy)

On Thursday, September 21: U.S. Chargé d’Affaires Dr. Inmi Patterson and Dr. Leonard Akwilapo pose for a group picture with Peace Corps Volunteers moments after the swearing-in ceremony in Dar es Salaam. The American volunteers will work in the education field in 27 districts in Tanzania. (Photo: courtesy of U.S. Embassy)
………………………………………………………………………..
, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Inmi Patterson aliwaapisha wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps wapatao 57 kuhudumu nchini Tanzania katika kipindi cha miaka miwili katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Peace Corps jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa Kimarekani watakaofanya kazi katika sekta ya elimu watapangiwa kuhudumu katika wilaya za Iringa, Mufindi, Same, Kyela, Masasi, Maswa, Singida Vijijini, Lushoto, Chamwino, Hai, Rombo, Wete, Rungwe, Njombe, Iringa Vijijini, Sumbawanga, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Hanang, Mbeya, Nachingwea, Hanang, Iramba, Kiomboi, Mbeya Rural, Shinyanga na Singida Mjini.
Mgeni rasmi katika hafla hii alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Leonard D. Akwilapo. Hafla hii ilihudhuriwa pia na wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps wanaoendelea kuhudumu na wale waliohudumu hapo zamani pamoja na maafisa kutoka mashirika mengine yanayojihusisha na wafanyakazi wa kujitolea. Akizungumza na wafanyakazi hao wa kujitolea Kaimu Balozi Patterson alisema: “Wakati ambapo kuna uwezekano kwamba mnaweza kuwa Wamarekani wa kwanza kuishi na wafanyakazi wenzenu au majirani wa Kitanzania, ni wazi kwamba kwa Watanzania hao nyinyi mtaendelea kuwa wawakilishi wa Watu wa Marekani.”
Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa zaidi ya miaka 50, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:
Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao;
Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;
Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.
Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolewa wa Peace Corps 2,500 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1961. Peace Corps hutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wenye utaalamu katika nyanja mbalimbali ambao hupangiwa kufanyakazi katika jamii wakifundisha katika shule za sekondari (hisabati, sayansi na Kiingereza), wakitoa elimu ya afya na utunzaji wa mazingira.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA PEACE CORPS WAPATAO 57 WAAPISHWA KUHUDUMU NCHINI KWA MIAKA MIWILI
WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA PEACE CORPS WAPATAO 57 WAAPISHWA KUHUDUMU NCHINI KWA MIAKA MIWILI
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/09/mar1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/wafanyakazi-wa-kujitolea-wa-peace-corps.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/wafanyakazi-wa-kujitolea-wa-peace-corps.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy