WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR

Wanajopo walioshiriki mjadala huo kutoka (kushoto) ni Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks, Given Edward toka mtandao wa MyEl...


Wanajopo walioshiriki mjadala huo kutoka (kushoto) ni Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks, Given Edward toka mtandao wa MyElimu, Kiya JK wa taasisi ya
SEMA na  Irene Kiwia wa
TWA network
Mmoja wa wachangiaji Bw. Yeriko Nyerere  akichangia jambo wakati wa siku hiyo.

 Bw. Paschal Masalu kutoka Elimika Wikiendi akiendelea ku Tweet wakati wa Siku hiyo ya kisomo.

Baadhi ya wadau mbalimbali wa Elimu wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kisomo

Wadau mbalimbali wa elimu wamekutana kuadhimisha siku ya kimataifa ya
kisomo ambayo hufanyika Septemba 8 kila mwaka. Maadhimisho hayo
yaliyoandaliwa na taasisi ya iSwapMyBooks kwa kushirikiana na SOMA pia
Elimika Wikiendi ulihusisha mjadala wa namna ambavyo Tanzania inaweza
kutumia faida ya uwepo wa nyenzo za kidigitali katika kusaidia watoto na
watu wazima kujifunza.



Akifungua maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji
wa taasisi ya SOMA Bi. Demere Kitunga alieleza namna ambavyo kwa miaka ya
karibuni Tanzania imekuwa ikipiga hatua katika matumizi ya nyenzo za
kiditali kutokana na usambaaji wa matumizi ya vifaa vilivyounganishwa na
mtandao wa intaneti hivyo kupelekea uhitaji katika kutumia nyenzo hizi
katika kuboresha namna ambavyo watoto wanaweza kujifunza masomo.



Wanajopo walioshiriki mjadala huo Irene Kiwia wa
TWA network, Given Edward toka mtandao wa MyElimu, Kiya JK wa taasisi ya
SEMA na Viola Julius mratibu wa tovuti ya iSwapMyBooks walielezea namna
ambavyo taasisi zao zimekuwa zikitumia njia za kidigitali kuwahamasisha
watoto na vijana  kujifunza kwa kubadilishana ujuzi kupitia mtandaoni.



Washiriki wengine kwa namna tofauti walionyesha
wasiwasi kwa namna ambavyo utaratibu wa watu kujisomea unaendelea
kutoweka na hasa kwa wazazi ambao wamekuwa hawana utaratibu wa
kuwanunulia watoto vitabu badala yake kuwapa simu za mkononi ambazo
wamekuwa wakizitumia kwa mambo yasiyofaa. Akijibu wasiwasi huo,
Mkurugenzi wa taasisi ya SEMA ndugu Kiiya JK alisema ni wakati mitaala
ya masomo ibadilike kuendana na hali halisi. “Tunalazimika kama
Watanzania kutengeneza vitabu vinavyoendana na hali halisi ya maisha
yetu kwa sasa, wenzetu wamegundua hilo na wamekuwa mstari wa mbele
kuwekeza katika kuchapisha vitu vinavyowafaa watoto wetu”.

Siku ya kimataifa ya kisomo ilianzishwa na
shirika la UNESCO miaka 50 iliyopita ambapo kaulimbiu ya mwaka huu
ilikuwa “Kisomo Katika Ulimwengu wa Kidigitali”.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR
WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KISOMO,JIJINI DAR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPRU7lkLaN16JZW5u0XX9DNnX0BHbgLMsIZ6nuim0N4p_aM80dRPvIqEMSMnffdW6RGIUv8ouAMjpBggydf1T8WK4hpStjytfeytRt8JLRxt7ztraf5kXyWakjDFRGFjDhFeuzF3VJHUs/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPRU7lkLaN16JZW5u0XX9DNnX0BHbgLMsIZ6nuim0N4p_aM80dRPvIqEMSMnffdW6RGIUv8ouAMjpBggydf1T8WK4hpStjytfeytRt8JLRxt7ztraf5kXyWakjDFRGFjDhFeuzF3VJHUs/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/wadau-wa-elimu-wakutana-kuadhimisha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/wadau-wa-elimu-wakutana-kuadhimisha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy