THBUB YAMPONGEZA RAIS KWA TAMKO KUHUSU KUTOTEKELEZA ADHABU YA KIFO

- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 213...



-
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Tovuti: www.chragg.go.tz


Septemba 12, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


THBUB yampongeza Rais kwa tamko kuhusu kutotekeleza adhabu ya kifo


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea tamko la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Septemba 11, 2017 kuhusu kutotekeleza adhabu ya kifo wakati wa uongozi wake, kuwa ni tamko lenye kuzingatia haki ya msingi ya kuishi.


Tume inapenda kuungana na wadau wengine kumpongeza Mhe. Rais kwa tamko hilo ambalo limekuja muda mfupi kabla ya Siku ya Kimataifa ya kuhamasisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuta adhabu ya kifo, ambayo huadhimishwa Oktoba 3 ya kila mwaka.  


Uamuzi wa Mhe. Rais unaendana na Mkataba wa Kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayozitaka nchi wanachama kufuta au kusimamisha utekelezaji wa adhabu ya kifo (abolition/moratorium on the death penalty).


Tume inatambua kwamba adhabu ya kifo haijatekelezwa hapa nchini katika kipindi cha takriban miaka 20 iliyopita na hivyo kudhihirisha kwamba Tanzania ni nchi isiyotekeleza adhabu ya kifo kwa hiari yake yenyewe pamoja na uwepo wa adhabu hiyo katika sheria za nchi.


Kwa kuzingatia kauli ya Mhe. Rais pamoja na mahitaji ya sheria za kimataifa za haki za binadamu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapenda kuchukua nafasi hii, kuishauri Serikali iridhie Itifaki ya pili ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa; Itifaki ambayo inazitaka nchi wanachama kufuta adhabu ya kifo.


Imetolewa na:
(SIGNED)


Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti


TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA


Septemba 12, 2017


Bahame Tom Nyanduga

Mwenyekiti


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: THBUB YAMPONGEZA RAIS KWA TAMKO KUHUSU KUTOTEKELEZA ADHABU YA KIFO
THBUB YAMPONGEZA RAIS KWA TAMKO KUHUSU KUTOTEKELEZA ADHABU YA KIFO
https://lh3.googleusercontent.com/6GeidKA1Xud77_WRwjI_JmJ1_EdDuDWARXwoFhd1mQGgp-9TARlvk9I78_9ID3pxe8RFhuGL23Phx8ZtplbttKUEmq9tszNys1CHqh6qm3nhk4vwiPJNJpIf3qBt3Q-XYjuWk523NriSdDN2uw
https://lh3.googleusercontent.com/6GeidKA1Xud77_WRwjI_JmJ1_EdDuDWARXwoFhd1mQGgp-9TARlvk9I78_9ID3pxe8RFhuGL23Phx8ZtplbttKUEmq9tszNys1CHqh6qm3nhk4vwiPJNJpIf3qBt3Q-XYjuWk523NriSdDN2uw=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/thbub-yampongeza-rais-kwa-tamko-kuhusu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/thbub-yampongeza-rais-kwa-tamko-kuhusu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy