SHINDANO LA MR TANZANIA KUFANYIKA DESEMBA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Paschal Dotto-MAELEZO Chama cha Watunisha Misuli Tanzania (TBBF) kimetangaza kuwa mashindano ya Mr. Tanzania, Style, I...







Na Paschal Dotto-MAELEZO
Chama cha Watunisha Misuli Tanzania (TBBF) kimetangaza kuwa mashindano ya Mr. Tanzania, Style, Icon yaani, Mr handsome pamoja na Mr Photogenic yanatarajiwa kufanyika Disemba 16, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Mr. Tanzania na Mkurugenzi wa Pilipili Entertainment Nilesh Bhatt akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu mashindano ya Mr. Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 16 katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). (Picha na Robert Okanda Blogspot)


Mwenyekiti wa Shirikisho la Wajenga Misuli Tanzania (TBBF) Nemes Chiwalala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya Mr. Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Desemba 16 leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo na Mkurugenzi wa Pilipili Entertainment Nilesh Bhatt, Msemaji wa Pilipili Entertainment Mohamed Ollotu (Mzee Chillo) na Katibu wa TBBF Francis Mapugilo.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam, leo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Francis Mapungilo alipozungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati ya kuuendeleza mchezo wa kutunisha misuli hapa nchini.
Alisema mchezo wa kutunisha misuli ni kama michezo mingine ambayo inaongeza ajira kwa vijana hivyo amewataka vijana kuichangamkia fursa hiyo kwani kwa sasa wameimarisha zaawadi tofauti na hapo awali.
“Mashindano yatakuwa yakioneshwa mubashara kupitia chaneli ya Azam 2 hivyo akawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo huo kuangalia kupitia luninga zao, hii pia itaongeza chachu kwa wanamichezo”, alisema Bw. Mapungilo.
Bw.Mapungilo aliwataka washiriki kuzingatia na kuzielewa kanuni za mchezo huo ili waweze kuchaguliwa kwani miongoni mwa vigezo vitakavyotumika ni kujua taratibu na kanuni za mchezo huo.
Alibainisha kuwa mchakato wa mchujo utaanza Desemba 12, 2017 na huu utakuwa mchujo wa kwanza kutoka kwenye kundi kubwa la washiriki 1000 ambapo katika mchujo huo watatakiwa washiriki 100.
Aidha Bw.Mapungilo alieleza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuwa ya haki kwani Majaji  watapewa semina mahususi kuhusu taratibu za mashindano pamoja na Sheria zinazosimamia mchezo huo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa (TBBF) Bw.Nemes Chiwalala alisema wanataka kufanya mchezo huo kuwa chanzo cha kipato na ajira kwa vijana kwani mashindano hayo yanafanyika  dunia nzima ambapo mwaka jana mshindi alitoka India.
Aidha Bw. Chiwalala amezungumzia kuwa watakuwa na zawadi nono kwa washindi watatu ambapo mshindi wa kwanza atapata gari aina ya Noah na fedha za kitanzania shilingi 10,000,000 huku mshindi wa pili akichukua 5,000,000 wakati mshindi wa mwisho atapata shilingi 2,500,000.
Kwa upande wa mashindano ya (Mr.handsome na Mr.photogenic na style) Bw. Chiwalala alibainisha kuwa zawadi nono zimeandaliwa kwaajili yao ili kuleta hamasa kwa watanzania waweze kuupenda na kushiriki katika mchezo huo.
Mwigizaji mkongwe nchini Mzee Chillo ambaye ni Msahauri wa kampuni ya ya filamu ya Pilipili, alisema wameamua kuingia mkataba wa miaka mitano na TBBF kwaajili ya kuendeleza mchezo huo nchini Tanzania lengo likiwa kuhakikisha wanatoa washiriki watakaoshiriki katika mashindano ya Dunia yaani Mr. World.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SHINDANO LA MR TANZANIA KUFANYIKA DESEMBA JIJINI DAR ES SALAAM
SHINDANO LA MR TANZANIA KUFANYIKA DESEMBA JIJINI DAR ES SALAAM
https://i.ytimg.com/vi/hytIx6zbgTU/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/hytIx6zbgTU/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/shindano-la-mr-tanzania-kufanyika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/shindano-la-mr-tanzania-kufanyika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy