SBL YAZINDUA BIA MPYA YA PILSNER KING

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (kulia) Mjumbe  wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Christopher Gachuma (kushoto) na ...




Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (kulia) Mjumbe  wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Christopher Gachuma (kushoto) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka, wakigonga chupa za kinywaji kipya cha Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza mapema usiku wa jana .



Mhudumu akiweka chupa ya Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza juzi.










Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (katikati) akiwa amevaa vazi la mfalme baada ya kuzindua bia mpya ya Pilsner King jijini Mwanza juzi, Mjumbe wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti (SBL) Bw.Christopher Gachuma (kulia) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka.





Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(katikati)akiwa amevaa vazi la mfalme baada ya kuzindua bia mpya ya Pilsner King jijini Mwanza juzi, Mjumbe wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Christopher Gachuma (kulia) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka.



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella (kulia) Mjumbea wa Bodi wa Kampuni Ya bia ya Serengeti (SBL) Chacha Gachuma(kushoto) na  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka, wakionja kinywaji kipya cha Pilsner King wakati wa uzinduzi jijni Mwanza mapema jana usiku.




Muonekano wa Chupa 



Wagon waalikwa wakiwa wanafuatilia shughuli za uzinduzi.




Muda wa kuonja ladha ya Pilsner King mara baada ya uzinduzi mapema jana usiku katika Hotel.



Wagon waalikwa wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa pilsner king 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa katika picha ya pamoja na mwageni waalikwa mara baada ya   uzinduzi wa pilsner king mapema jana usiku Jijini Mwanza.



Mwanza, Septemba 20, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua bia mpya
inayojulikana kama Pilsner King ambayo ni mwendelezo wa bia ya Pilsner Lager iliyozoeleka na ambayo ipo sokoni kwa kipindi kirefu.

Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa bia hiyo jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL
Cesear Mloka aliielezea bia hiyo mpya kama bia imara ambayo itakuwa kipenzi cha
wanaume jasiri na wanaojiamini.

Bia ya Pilsner King ina kilevi cha asilimia 7.6%, na ndiyo bia imara kuliko zote
zinazozalishwa hapa nchini.

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, Pilsner King imetengenezwa na mzalishaji bia wa
Kitanzania kwa kanuni za kimataifa akitumia malighafi za hapa nchini zenye
ubora wa hali ya juu ambazo zimeipa bia hiyo ladha murua. “Hii ni kama zawadi
kwa wanaume wa kweli baada ya shughuli nyingi za mchana kutwa,” anasema Mloka

Kwa mujibu wa
mkurugenzi huyo, bia ya Pilsner imepata jina lake kutoka katika mji wa Pilsen
uliopo Jamuhuri ya Czech ambako bia hiyo ilitengenezwa kwa mara ya kwanza na
kuongeza kuwa, bia hiyo ya kipekee na yenye ladha ya aina yake itakuwa ni
chaguo sahihi kwa wateja wanaopenda kuwa ‘wanaume wa kweli’

 “Ikiwa na kilevi cha asilimia 7.6% Alc,
Pilsner King, ambayo kauli mbiu yake ni ‘Kutana na Mfalme, kwa ajili ya Wanaume
Imara na Wenye Ujasiri’, imetengenezwa kwa kuzingatia kanuni halisi za
utengezaji wa bia ya kwanza ya Pilsner iliyotengenezwa huko Ulaya Mashariki,”
anaeleza Mloka

Uzinduzi huo Ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, ambaye aliisifia kampuni ya SBL kwa kuonyesha njia katika ubunifu wa vinywaji vyenye kileo hapa nchini.

Mongela pia aliipongeza SBL kwa kufanya uwekezaji Mkoani Mwanza kupitia kiwanda chake cha bia ambacho amesema kimekuwa kikichangia maendeleo ya kiuchuni ya mkoa huo.

“Napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya wananchi wa  Mwanza kwa kampuni ya SBL. Uwekezaji wao hapa Mwanza umesaidia upatikanaji wa  ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja pamoja na fursa za kibiashara kwa
wakazi wa jiji hili,” alisema Mongela.

Pamoja na
kiwanda cha Mwanza, SBL ina viwanda vingine viwili vya bia, kimoja kipo jijijni
Dar es Salaam na kingine kipo Moshi mkoani Kilimanjaro. SBL inazalisha bia kama
vile  Pilsner Lager, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness Stout and bia inayobeba
bendera ya kampuni, Serengeti Premium ambayo imeshinda zaidi ya medali 10 za
kitaifa na Kimataifa.




































































































COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SBL YAZINDUA BIA MPYA YA PILSNER KING
SBL YAZINDUA BIA MPYA YA PILSNER KING
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfbuz629jj8O301fvCig8zyhgMBoUgQdDrec3G849fZZfSTr8iTmKxaqb8R5sNhQr1IiFZcfu5SDLKvVGX4r4oSzjQ4PY7wSXCOW3Uj0ukJfQF_F-ZGIyEG4PJSUOfLhyI_ozPejjsyko/s640/cheers+%25282%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfbuz629jj8O301fvCig8zyhgMBoUgQdDrec3G849fZZfSTr8iTmKxaqb8R5sNhQr1IiFZcfu5SDLKvVGX4r4oSzjQ4PY7wSXCOW3Uj0ukJfQF_F-ZGIyEG4PJSUOfLhyI_ozPejjsyko/s72-c/cheers+%25282%2529.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/sbl-yazindua-bia-mpya-ya-pilsner-king.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/sbl-yazindua-bia-mpya-ya-pilsner-king.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy