RAIS DKT MAGUFULI AMJULIA HALI MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA ALIYEJERUHIWA KWA RISASI
HomeJamii

RAIS DKT MAGUFULI AMJULIA HALI MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA ALIYEJERUHIWA KWA RISASI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Bri...

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE (JMKF) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
DK. KIGWANGALLA AITAKA KAMATI INAYOCHUNGUZA TUHUMA ZA MAUAJI YA TEMBO KATIKA IKOLOJIA YA RUGWA-RUAHA KUTENDA HAKI
MPINA AWABANA WANAOTOROSHA PUNDA KWENDA NJE YA NCHI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba akielezea alivyoshambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na mguuni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu)


ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) wakioneshwa na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe Brigedia baadhi ya risasi zilizotolewa kwenye mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba baada ya kushambuliwa wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Brigedia Jenerali Dkt. Paul Massawe, Brigedia Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba na wauguzi wakiomba dua wakiongozwa na Mama Margareth Vicent Mritaba hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa Meja Jenerali Mritaba akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mtoto Nathan Martin wakati akitoka kumjulia hali Meja jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati anaingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Aloys Konolipa wa Shule ya Msingi Kidugalo wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani alipopita kuwapa pole wagonjwa wengine baada ya kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vicent Mritaba aliyelazwa Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam alikolazwa akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa risasi mkononi, tumboni na kiunoni wakati akiingia nyumbani kwake Ununio wilaya ya Kinondoni. Picha na IKULU.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Septemba, 2017 ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Meja Jen. Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.Meja Jen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua ili apone haraka.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen. Venance Mabeyo pia ametembelea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.

Mhe. Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya Jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI AMJULIA HALI MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA ALIYEJERUHIWA KWA RISASI
RAIS DKT MAGUFULI AMJULIA HALI MEJA JENERALI MSTAAFU VICENT MRITABA ALIYEJERUHIWA KWA RISASI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMXFtnR_a2etcGNj78eCyaZjwEwttkJJlohcM8U5c1DHXWVCKc1ym1-gBUx5MQ9zU3TiHfZeIZiav8V4fnWg6njDbeGsZI8gsO_876xzdnmyKjaziH3n5KPJ4rpV-HACwIU_BVA9Ep6vm7/s640/LU+%25287%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMXFtnR_a2etcGNj78eCyaZjwEwttkJJlohcM8U5c1DHXWVCKc1ym1-gBUx5MQ9zU3TiHfZeIZiav8V4fnWg6njDbeGsZI8gsO_876xzdnmyKjaziH3n5KPJ4rpV-HACwIU_BVA9Ep6vm7/s72-c/LU+%25287%2529.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/rais-dkt-magufuli-amjulia-hali-meja.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/rais-dkt-magufuli-amjulia-hali-meja.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy