RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, AAGANA NA BALOZI WA CHINA AONANA NA MZEE BUTIKU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
HomeJamii

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, AAGANA NA BALOZI WA CHINA AONANA NA MZEE BUTIKU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz To...

NAFASI SCACE WAJA NA HARAMBEE YA KUCHANGIA 'GALLERY' YA MPYA NA ENEO LA SANAA KWA WATOTO
WAZIRI MKUU MAJALIWA ASEMA TATIZO LA UMEME LINDI NA MTWARA KUWA HISTORIA, MRADI WA UMEEM WA TANESCO MAHUMBIKA NI MKOMBOZI
MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI KUFANYIKA KESHO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bw. Jose Graziano da Silva amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Shirika hilo lipo tayari kushirikiana na Tanzania kufanya mageuzi katika kilimo kwa kuwezesha uzalishaji wa mazao na viwanda vya mazao hayo.
Bw. Jose Graziano da Silva amesema hayo leo tarehe 06 Septemba, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli na kumshukuru kwa ushirikiano mzuri ambao shirika hilo limeupata kwa kipindi cha miaka 40 ya uwepo wake hapa nchini.
Akitoa mfano wa nchi yake ya Brazil Bw. Jose Graziano da Silva amesema Tanzania inaweza kupata manufaa makubwa ya kuongeza uzalishaji wa chakula, kuuza nje ya nchi, kuzalisha ajira na kukuza pato la Taifa kupitia mapinduzi yatakayotokana na kuunganisha kilimo na viwanda vikiwemo vya kusindika nyama na samaki kwa kuwa fursa zipo nyingi.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Bw. Jose Graziano da Silva kwa kuja nchini na amemhakikishia kuwa Serikali itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake FAO, huku akitilia mkazo dhamira yake ya kutaka ushirikiano huo uelekezwe katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.
“Tanzania ina maziwa mengi, ina ukanda wa bahari wenye urefu wa kilometa 1,422 na ina mito mingi ambayo inaweza kuwekezwa viwanda vya samaki, inashika nafasi ya pili kwa mifugo Barani Afrika, hivyo tunahitaji kujenga viwanda vya nyama.
“Asilimia 75 ya nguvu kazi ya Taifa ni vijana ambao wanauwezo wa kuzalisha mazao mengi ya kilimo tunahitaji viwanda, uchumi wetu ni mzuri na unakua kwa wastani wa asilimi 7.1 na mengine mengi, kwa haya yote tunahitaji wadau ikiwemo FAO tushirikiane kutumia fursa hizi” amesema Mhe. Rais Magufuli na kuahidi kuwa Serikali yake imejipanga kusimamia miradi yoyote itakayoletwa nchini ili itekelezwe kwa uadilifu na ubora wa hali ya juu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo hayo Mzee Butiku amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuongoza Serikali ambapo katika kipindi kifupi amesimamia vizuri nidhamu, watu kufanya kazi, kupiga vita rushwa, ulipaji wa kodi na amemtaka asirudi nyuma kwa kuwa nchi inakwenda vizuri.
“Mimi nimefanya kazi hapa Ikulu kwa miaka 23, Mwl. Nyerere alijenga misingi mizuri, lakini huyu Rais Magufuli ameisimamia vizuri sana, unapofanya mambo kama haya, lazima hapa nyumbani na huko nje kutakuwa na maneno, mazuri sikiliza, ya hovyo achana nayo” amesisitiza Mzee Butiku.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli ameagana na Balozi wa China hapa nchini anayemaliza muda wake Mhe. Dkt. Lu Youqing na kumshukuru kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli amesema katika kipindi chake Mhe. Dkt. Lu Youqing ametoa mchango mkubwa katika kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano kati China na Tanzania, uliofanikisha kuongeza uwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, elimu, kilimo, afya na kukuza biashara ambapo wafanyabiashara wengi wa China wamekuja kuwekeza nchini, mambo ambayo yamezalisha ajira na kukuza pato la nchi.
Mhe. Dkt. Magufuli amemuomba Mhe. Dkt. Lu Youqing kuendelea kuitangaza vyema Tanzania nchini China, ambako anakwenda kushughulikia masuala ya uchumi na kwamba anaamini atatumia nafasi hiyo kuhimiza wawekezaji na wafanyabiashara wengi zaidi wa China kuja kuwekeza hapa nchini.
“Mhe. Balozi Dkt. Lu Youqing Watanzania hatutakusahau kwa mchango wako, wewe ni ndugu na rafiki yetu, tunakushukuru sana kwa yote uliyoifanyia nchi yetu, naomba nikuhakikishie kuwa kazi nzuri uliyoifanya tutaiendeleza na tutashirikiana na Balozi mpya atakayekuja kuendeleza pale ulipoachia” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Dkt. Lu Youqing amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwa Balozi mzuri wa kuinadi Tanzania huko nchini China.
“Mhe. Rais Magufuli nakushukuru sana, hapa Tanzania ni nyumbani kwangu na nipo tayari wakati wote kutoa ushirikiano pale nitakapohitajika kufanya hivyo kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini China ama kutoka Serikalini hapa Tanzania” Amesema Dkt. Lu Youqing.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Septemba, 2017




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini Bw. Fred Kafeero na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. alipokutana naye Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Meshack Malo Ofisa Mwambata wa FAO kutoka Roma Italia aliyeongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu na kadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, AAGANA NA BALOZI WA CHINA AONANA NA MZEE BUTIKU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, AAGANA NA BALOZI WA CHINA AONANA NA MZEE BUTIKU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
https://lh5.googleusercontent.com/-Juza-HFFf2lIUWXPGClQCJbbLCBAICxZwJhG19c2bpIaNiwnIc0RQsjdBI3gQ9haqJ7foSjg9ij0zWh1RlWO0EebZdGNJ7L2KQX_nGeSf9kqtcq-jxZCkaw7z-Ubxt5h3OQKW6n3-nalXFHig
https://lh5.googleusercontent.com/-Juza-HFFf2lIUWXPGClQCJbbLCBAICxZwJhG19c2bpIaNiwnIc0RQsjdBI3gQ9haqJ7foSjg9ij0zWh1RlWO0EebZdGNJ7L2KQX_nGeSf9kqtcq-jxZCkaw7z-Ubxt5h3OQKW6n3-nalXFHig=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/rais-dkt-magufuli-akutana-na-mkurugenzi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/rais-dkt-magufuli-akutana-na-mkurugenzi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy