MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA VALERIE NDENEINGO AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA RADIO NA TELEVISION ZA MTANDAONI ( ONLINE RADIO NA TELEVISION) DAR
HomeJamii

MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA VALERIE NDENEINGO AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA RADIO NA TELEVISION ZA MTANDAONI ( ONLINE RADIO NA TELEVISION) DAR

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Valerie Ndeneingo akiongea na wamiliki wa Radio na Television za M...

WATANZANIA WASHINGTON DMV- WAIRUDISHA LABOR DAY WEEKEND REUNION KWA KISHINDO
TRA YAENDELEA KUWABAMBA WASIOTOA RISITI ZA MACHINE ZA KIELEKRONIKI
MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA PROPERTY INTERNATIONAL, MAONYESHO YA SABASABA




Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Valerie Ndeneingo akiongea na wamiliki wa Radio na Television za Mtandaoni (On line Radio and Television) kwenye Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano, jijini Dar Es Salaam tarehe 13, September 2017
Ndugu Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
Wamilikiwa Radio naTelevisheni za Mtandaoni (on line Radio &Televisheni),
Wadau wa habari,
Awali ya yote naomba nianze kwa Kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutupa uzima na kutuwezesha kukutana kwenye mkutano huu muhimu unaozungumzia masuala ya Mawasiliano na huduma zinazotolewa n avyombo vyetu vya habari.
Vilevile naomba nichukue fursa hii kuwa shukuru kwa kuitikia wito na mchango wenu mkubwa mnaoutoa kupitia vyombo vyenu mbalimbali vya Mawasiliano kama vile online Radio, online televisheni, blogs na vinginevyo. Vyombo hivi ni matokeo ya ukuaji wa kasi wa teknolojia ya habari, nani fursa nzuri kwa wanahabari kutoa na kusambaza habari mbalimbali zinazohusu jamii inayotuzunguka.
Ni miaka takribani mitano tuiliyopita, kulikuwa hakuna fursa hizi za kupata matangazo ya televisheni kupitia kwenye mitandao, na kama ilikuwepo, ubora wa picha ulikuwa hafifu. Lakini sasa huduma hii imeenea kwa Watanzania wengi, na hivyo kuwepo na umuhimu wa kuisimamia huduma hii ipasavyo ili iwezekuleta tija kwenye taifa na si vinginevyo.
Mchango wenu kupitia huduma hizo sio tuunaelimisha watumiaji bali pia unatoa mwanga na fursa mbalimbali ambazo Watanzania wanaweza kuzitumia kujiimarisha kiuchumi.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kupitia Kamati yake ya Maudhui inatambua na kuthamini sana kuwepo kwa fursa hii ya upashanaji wa habari. Na ni kwa kuzingatia umuhimu huo Serikali iliamua kuruhusu huduma kama vile online Radio, online televisheni na blogs ziendelee kutolewa wakati miongozo na taratibu stahiki zikikamilishwa.
Ndugu Wanahabari,
Mkutano wetu wa leo, umelenga kuzungumzia namna bora ya upashanaji wa habari na utangazaji wa matukio mbalimbali yanayotokea (current affairs) kupitia “vyombo vya habari mtandaoni” (On line media).
Ndugu Wanahabari,
Kama mnavyofahamu, TCRA, pamoja na mambo mengine, imepewa dhamana ya kisheria kusimamia maudhui katika vyombo vya Utangazaji na vile vyaki-elekroniki. Jukumu hili, linaifanyaTCRA kuhakikisha kuwa inakuwa karibu na watoa huduma na watumiaji wa vyombo hivi na kujiridhisha kuwa vyombo hivi vinatumika kwana mna bora iliyokusudiwa katika jamii. Niendelee kusematuku wa TCRA inatambua umuhimu wa vyombo vya habari kupitia mitandao (online media) ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii katika kuboresha maisha ya Watanzania na kuleta maendeleo.
Ni kwa ajili hiyo, leo tumeona ni vyema kukutana na wadau wahabari kupitia mitandao na wengineo, ilituweze kupeleka na kufikisha ujumbe kwa watumiaji wa huduma za mitandao kwa mustakabali wa nchi yetu, Amani ya nchi yetu na mafanikio ya kila mtu, mmoja mmoja, na ya nchi kwa ujumla kwamba yako mikononi mwenu.
Ndugu Wanahabari,
Baada ya kutoa Utangulizi huo, nianze kwa kutoa maangalizo machache yafuatayo kwa watoa huduma za habari, hususani kupitia mitandao:
Ni wajibu wetu kufahamu kuwa, sikila habari tunayoipata kutoka kwa jamii inafaa kusambazwa kwa jamii. Maadili ya Uandishi tunayotumiana kuzingatia kwenye vyombo vya Utangazaji wa Radio na Televisheni yanapaswa kutumika kwenye usambazaji wahabari kupitia mitandao. Tuelewe kuwa kuna habari zingine hazina tija kwa jamii, na zingine huleta uchochezi. Ni wajibu wetu kama wadau na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhakikisha kuwa tuna habarisha hukut ukizingatia kuwa habari zetu zinajenga umoja wa kitaifa, mshikamano na ushirikiano baina ya Watanzania bila kujenga hofu, kuchochea chuki na uhasama baina ya Watanzania.
Tungependa ieleweke kuwa kutumia mitandao ya  kijamii kutoa habari hakuondoi umuhimu wakufuata maadili ya uandishi na upashanaji wa habari.
Maadiliya Uandishi yanatutaka kuheshimu utu wa kila Mtanzania. Mambo ya ndani ya mtu binafsi na yaki-familia, hayapaswi kusambazwa kwenye vyombo vya habari vya mitandaoni. Hii inaondoa heshima na Utu wa mtu. Habari yoyote ya mtu binafsi haipaswi kutangazwa isipokuwa pale ambapo italazimika kwa maslahi ya umma mambo hayo yatangazwe na vyombo husika.
Matumizi ya Lugha
Ndugu wanahabari,
Vyombo vya Habari kupitia mitandao vimekuwa mstari wa mbele kupotosha lugha yetu ya Kiswahili, na vilevile kutumia lugha chafu zisizo na staha kwa jamii. Tukumbuke kuwa, habari na matumizi ya lugha chafu mtandaoni kwa sasa yanasambaa kwa kasi kubwa, ikizingatiwa kuwa watumiaji wa mitandao wanaongezeka siku hadi siku. Hii ni kwa sababu matukio mengi yanapotokea, huwafikia wananchi mapema zaidi.
Ni vyema tukawa makini katika kuchagua maneno na kuwa na matumizi sahihi ya lugha kwa ajili ya kuwa habarisha wananchi wetu maana matumizi ya lugha chafu haya tavumiliwa hata kidogo.
Vyanzo na Usambazaji wa Habari na Matukio
Ndugu wana habari,
Sote tunashuhudia kuwa Teknolojia ya Habari mtandaoni, imetoa fursa kwa mtu yeyote kuwa chanzo cha habari. Kwa mfano; baadhi ya watumiaji wa mitandao wamekuwa vyanzo vya Habari, kwa kutengeneza habari wenyewe, kwa kujirekodi (clips) na kusambaza mitandaoni habari(clips) hizo. Wengine wamekuwa wakipiga picha na kurekodi matukio mbalimbali na baadaye kuyasambaza mitandaoni.
Kuwa chanzo cha habari na kusambaza matukio ni jambo ambalo linatakiwa lifanywe kwa tahadhari kubwa. Ikumbukwe kuwa maadili ya uandishi wa Habari hayaruhusu kusambaza picha kama zile zitokanazo na matukio ya ajali zikionyesha utupu wa mtu aliyepata ajali na damu ambapo huleta hofu kwa jamii.
Naomba kuwakumbusha na kuwatahadharisha kuwa ni kosa la jinai kwa chanzo chochote cha habari na usambazaji wa habari za matukio iwapo maudhui yake ni yale yasiyofaa.
Mwisho nawashukuru sana nyote.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA VALERIE NDENEINGO AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA RADIO NA TELEVISION ZA MTANDAONI ( ONLINE RADIO NA TELEVISION) DAR
MWENYEKITI WA KAMATI YA MAUDHUI YA TCRA VALERIE NDENEINGO AZUNGUMZA NA WAMILIKI WA RADIO NA TELEVISION ZA MTANDAONI ( ONLINE RADIO NA TELEVISION) DAR
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/09/DSC01197.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/mwenyekiti-wa-kamati-ya-maudhui-ya-tcra.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/mwenyekiti-wa-kamati-ya-maudhui-ya-tcra.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy