MEYA WA JIJI LA DAR ASITISHA MKATABA NA KAMPUNI YA UKUSANYAJI USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI
HomeJamii

MEYA WA JIJI LA DAR ASITISHA MKATABA NA KAMPUNI YA UKUSANYAJI USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesitisha mkataba na Kampuni ya Mwamkinga Auction Mart and Brokers ambayo ilikuwa inashughulika na kud...

UBALOZI WA KUWAIT YAWAPAIGA TAFU WENYE ULEMAVU WA MKOA WA TABORA KUPITIA DK. MKOGA
TANZANIA NA UGANDA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUBORESHA SEKTA YA MIFUGO
KANISA LA UKOMBOZI LATEMBELEA AMANI, LAKUMBUSHA KUJALI WATOTO





Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesitisha mkataba na Kampuni ya Mwamkinga Auction Mart and Brokers ambayo ilikuwa inashughulika na kudhibiti maegesho ya magari katika maeneo yasiyosahihi Kanda ya Temeke.


Akiongea leo na waandishi wa habari ofisini kwake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema Mkandarasi huyo amevunja masharti ya mkataba kutokana na kufanya kazi zake bila kuzingatia weledi.
“Wakandarasi wetu lazima waheshimu hawa Watanzania wanaotumia magari sio “ATM” nimesikia kelele nyingi sana kuhusu Mwamkinga jinsi anavyokamata malori kule, kimsingi anawaotea na kuwapiga faini kubwa pengine laki tatu hadi nne na watu wanakuwa wameegesha kwa dharura chini ya dakika 30 anawapiga faini”, amesema Mwita.
Mstahiki Meya ameongeza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeamua kusitisha mkataba huo kuanzia Septemba 19 kwasababu ameshapewa onyo lakini hawajaonesha nia ya kubadilika. Aidha Mwita amewataka Wakandarasi wengine waendelee kufanya kazi kwa weledi vinginevyo atavunja mikataba yao pia.
Amesema haiwezekani kwamba mtu amesimama kwa dakika moja alafu gari lake linafungwa kwa mnyororo na kumwandikia faini ya Sh 200,000 hadi Sh 300,000 ambayo haipelekwi halmashauri.
“Hiyo kampuni ilikuwa inafanya kazi hadi saa tatu usiku tofauti na makubaliano ya mkataba unavyosema mwisho saa 12 jioni . Nitaendelea kufuatilia kwa wilaya za Kinondoni na Ilala ambapo kama wataenda tofauti na mikataba inavyosema watasitishiwa mikataba yao” ameongeza.
Mwita amesema lengo la halmashauri siyo kumkandamiza mwananchi bali kusimamia sheria ili watu wazifuate lakini imeonekana tofauti ambapo amekiri kusikia watu hao wanakusanya hadi shilingi milioni nne kwa mwezi ambazo haziwasilishwi katika halmashauri ya jiji
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MEYA WA JIJI LA DAR ASITISHA MKATABA NA KAMPUNI YA UKUSANYAJI USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI
MEYA WA JIJI LA DAR ASITISHA MKATABA NA KAMPUNI YA UKUSANYAJI USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3x7b0Q8RdCpHlYyDYTqjO0GU8ik7_ZKQBIvYxgvTGj7WBBX8DM5xoRvm9I9KqPmScjwzkke17KJc-0Ypa-9KpouanmfxAsd8h8kt1SWLb_SYf8hZV_uWIdNG2ne2AVqcWXUpp4AmecS0/s640/IMG_5129.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3x7b0Q8RdCpHlYyDYTqjO0GU8ik7_ZKQBIvYxgvTGj7WBBX8DM5xoRvm9I9KqPmScjwzkke17KJc-0Ypa-9KpouanmfxAsd8h8kt1SWLb_SYf8hZV_uWIdNG2ne2AVqcWXUpp4AmecS0/s72-c/IMG_5129.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/meya-wa-jiji-la-dar-asitisha-mkataba-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/meya-wa-jiji-la-dar-asitisha-mkataba-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy