MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA KWENYE DVD PEMBA
HomeJamii

MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA KWENYE DVD PEMBA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed  Shikhan akizungumzia kukamatwa kwa madawa hayo. Mzigo wa madaw...

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
MAJENERALI WAPYA WAVISHWA VYEO MAKAO MAKUU, JWTZ
WAZIRI NAPE AJIUNGA NA PSPF, AWASIFU KWA HUDUMA ZA "MWENDO KASI"


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed  Shikhan akizungumzia kukamatwa kwa madawa hayo.
mad2
Mzigo wa madawa hayo
……………………………………………………………………………
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limemkamata mwanamke mwengine akiwa na jumla ya kete 969 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya DVD. Mwanamke huyo ambaye amekamatwa na wenziwe wawili wanaume katika maeneo ya PBZ Chake Chake anakuwa wa pili kukamatwa ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya Septemba 9 mwezi huu kukamatwa mwengine akiwa na jumla ya kete 3621. Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Madungu Chake Cheke Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shikhan Mohamed Shikhan amemtaja mwanamke huo ni Asha Mohamed Issa (30) mkaazi wa Wawi Chake Chake, huku wenzake wakiwa ni Ali Nyoro Tirima (32)wa Wawi na Salim Said Kombo 23 mkaazi wa Konde Wilaya ya Micheweni. Aidha Kamanda Shikhan amesema jeshi la polisi Mkoa wa Kusini Pemba tayari inayo majina ya mabaharia wanaofanya kazi katika meli zinazotoka Unguje kuelekea Pemba wanaotumiwa kusafirisha madawa ya kulevya na kuwataka kuacha vitendo hivyo kwani jeshi hilo linawafuatilia.
“Ni kwamba wito wangu kwa mabaharia wa meli zinazotoka Unguja kuja Pemba, tayari tunayo majina ya mabaharia wa meli zote MV Mapinduzi, meli za Bakhresa zote hao ndio ambao wanatoa msaada mkubwa kwa waleta madawa ya kulevya yanapita katika mikono yao,tunawajua na tunawafuatilia kwa karibu”
Aidha kamanda huyo amewawata amewataka wamilika wa makampuni kuwatahadharisha mabaharia wao, kuacha kutumiwa na wahalifu wa madawa ya kulevya wa bangi na unga wanaopeleka madawa ya kulevya kisiwani humo kwani watawakamata.
Kwa upande mwengine Kamanda Shekhan amewaonya  wanawake wanaojiingiza kufanya biashara za madawa ya kulevya kuacha kabisa biashara hizo na kutafuta nija halali za kujipatia kipato.
“Kweli huyu ni mwanamke wa pili kumkamata kwa mkoa wetu, lakini natoa wito kwa wanawake hiyo sio biashara ya kusema wanaweza wakapata utajiri , warudi nyuma watafute biashara  zinazokwenda na maadili ya biashara” Septemba 9 mwaka huu jeshi la Polisi Mkuu wa Kusini Pemba huko maeneo ya Mkoani Pemba ilifanikiwa kumkamata na kete 3621 Zuhura Ahmed Ali (29) wa Jadida na alifikiswa mahakamani kwa mara ya kwanza Septemba 14

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA KWENYE DVD PEMBA
MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA KWENYE DVD PEMBA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/09/mad1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/madawa-ya-kulevya-yakamatwa-kwenye-dvd.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/madawa-ya-kulevya-yakamatwa-kwenye-dvd.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy