Na Masanja Mabula – Pemba Katika mwendelezo wa operasheni wa utokomezaji wa madawa ya kulevya wa Jeshi la Polisi nchini hatimae Jeshi hilo m...
Na Masanja Mabula – Pemba
Katika mwendelezo wa operasheni wa utokomezaji wa madawa ya kulevya wa Jeshi la Polisi nchini hatimae Jeshi hilo mkoa wa Kusini Pemba jana limefanikiwa kumkamata kijana mwengine akiwa na jumla ya kete 241 zinazosadhaniwa kua ni madawa ya kulevya.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amemtaja kijana waliyemkamata kuwa ni Haji Balozi Hassan (35) ambae alikuwa kwenye gari ya abiria akitokea mkoani kuelekea micheweni.
Alisema katika gari hiyo askari walimtilia mashaka abiria huyo ndipo walipoamua kumpekua na kufanikiwa kumkamata na madawa hayo aliyokua nayo katika mifuko yake ya suruali.
” Mpaka hivi sasa yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi na leo tutampeleka mahakamani kusomewa kosa lake” alisema Kamanda Shehan
Kamanda Shehan ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kufanikisha kutokomeza madawa ya kulevya yanayoonekana kuwa ni tatizo katika jamii.
Tukio la kukamatwa Hassan ni tukio mfululizo wa watuhumiwa wa madawa hayo kukamatwa kisiwani Pemba ambapo juzi Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia mikononi mwanamke mmoja mkaazi wa Wete akiwa na kete 3621 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya katika maeneo ya mbuguani Mkoani.
COMMENTS