SPIKA Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, amewataka watanzania kutumia Mfuko wa...
SPIKA Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, amewataka watanzania kutumia Mfuko wa Taifa wa Bima hiyo ili kupata unafuu wa matibabu pindi wanapougua.
Wito huo alitoa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti huyo wakati alipozindua kitengo cha kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Kairuki.
Alisema, kutokana na gharama ya matibabu kupanda kila siku,kadi za bima ya afya zitasaidia kwa kiasi kikubwa
kupata unafuu wa matibabu kipindi mgonjwa anapokuwa hana fedha.
Makinda, alisema bima hiyo inatoa fursa kwa wanachama kupata huduma za matibabu katika hospitali wanazoona zinatoa huduma nzuri na kumjali mgonjwa.
“Vituo vyenye huduma ya NHIF vinapaswa kutibia wagonjwa kwa kuwajali , kuwapenda pamoja na kuwa wakarimu kwa wagonjwa kwani huduma hii inasaidia sana watu hasa wale
wanaougua magonjwa yenye kulipia gharama
kubwa,”alisema Makinda.
Aidha alisema ni watu wachache ambao wanauwezo
wa kujitibu bila bima ya afya lakini watu wengi wanategemea huduma hiyo kulingana na gharama kubwa za matibabu katika baadhi ya magonjwa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki Dk. Asser Mchomvu, alisema nchini Tanzania watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa yanayosababishwa na matatizo ya figo.
“Kwa hivi sasa ugonjwa huo umeonekana kuathiri kati ya
asilimia 7 hadi 13 ya watanzania, wengi wao wakiwa wagonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus)na shinikizo la
damu(Acute Kidney injury) ,”alisema.
Alisema kwa muda mrefu hospitali yao imekuwa
ikipokea wagonjwa wenye matatizo ya figo na kulazimika kuwapa rufaa kwenda nje ya hospitali hivyo kupitia kitengo hicho kitaweza kutibu wagonjwa 40 kwa siku.
Alisema kuwa kutakuwa na mashine 10 zenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa na hadi kufikia sasa wamepata kibali cha wizara husika ambapo miongoni mwa mashine hizo
ipo ya kuchuja damu itakayosaidia kuzuia uharibifu wa figo wa kudumu na wa muda hivyo kuokoa gharama.
Dk. Mchomvu, alisema hospitali hiyo inatarajia kuongeza idadi ya mashine ili kuweza kuwahudumia wagonjwa wengi pamoja na kutoa huduma ya kupandikiza figo na kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHJF), Anne Makinda (katikati), akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki (kushoto), wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali.
Mkurugenzi Mkuu wa Kairuki Hospitali Dk. Asser Mchomvu, akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali.

COMMENTS