Na Greyson Mwase, Dar es Salaam Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani ametaka wakandarasi wanaofanya kazi ya kukamilis...
Na Greyson Mwase, Dar
es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Dkt. Medard Kalemani ametaka wakandarasi wanaofanya kazi ya
kukamilisha ujenzi wa vituo vya kupozea umeme jijini Dar es Salaam kuongeza kasi
ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika baadhi ya
maeneo ya jijini Dar es Salaam
Dkt. Kalemani aliyasema hayo katika nyakati tofauti
tarehe 18 Septemba, 2017 katika ziara yake ya kukagua mradi wa uboreshaji umeme wa jiji la Dar es Salaam unaohusisha
ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme vilivyopo katika maeneo ya Mbagala, Gongo la
Mboto, Kurasini na kituo kipya cha Kigamboni.
Akiwa katika kituo cha
kupooza umeme cha Gongo la Mboto, Dkt. Kalemani
aliagiza mradi huo kukamilika
ndani ya siku 14 ikiwa ni pamoja na kubadili wasimamizi wa mradi kutokana na
waliopo sasa kufanya kazi kwa kususasua.
Katika hatua nyingine,
akiwa katika kituo cha Kurasini Naibu Waziri Kalemani aliagiza kubadilishwa kwa
kundi la wataalam kwenye ujenzi huo na kuelekeza kazi hiyo ikamilike ndani ya
siku Tano
“Ninawaagiza wote kwa
pamoja kufanya kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kwa wakati, wananchi
wamechoka na taarifa za kukatiwa umeme za mara kwa mara, lazima mpambane”
alisema Dkt. Kalemani.
Alisema Serikali ya
Awamu ya Tano imeweka mikakati ya kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya Umeme
wa uhakika na kwa gharama nafuu na kuvutia Wawekezaji nchini.
Naye Mbunge wa
Kigamboni aliyekuwepo kwenye ziara hiyo, Faustine Ndugulile alimshukuru Naibu
Waziri kwa ujio wake na kueleza kuwa tatizo la kukatika kwa Umeme mara kwa mara katika maeneo ya
Mbagala, Gongo la Mboto, Kigamboni, Kurasini limekuwa ni la muda mrefu na
kupelekea wananchi kukata tama.
Alisema wananchi katika
maeneo husika wanahitaji Umeme katika shughuli za uzalishaji mali na
kujiongezea kipato na kuongeza kuwa hata Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
linahitaji mapato kutoka katika maeneo husika.
Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Dkt. Medard Kalemani akitoa maelekezo katika ziara hiyo.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
Dkt. Tito Mwinuka.
|
Mbunge wa Kigamboni,
Faustine Ndugulile akieleza jambo katika ziara hiyo.
|
Mafundi wakiendelea na
ujenzi katika kituo cha kupozea umeme cha Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam
|
Mafundi wakiendelea na ujenzi katika kituo cha kupozea umeme cha Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. |
Meneja wa Vituo vya Kupozea
Umeme nchini, Mhandisi Izahaki Mosha akieleza hatua ya ujenzi wa kituo
cha kupozea Umeme cha Kigamboni katika ziara hiyo.
|
COMMENTS